loader
RC GABRIEL AISHUKURU WIZARA KUELIMISHA WAJASIRIAMALI

RC GABRIEL AISHUKURU WIZARA KUELIMISHA WAJASIRIAMALI

WIZARA ya Viwanda na Biashara imeshiriki katika Tamasha la Mawasiliano, Utalii, Utamaduni na Maonesho ya Biashara, yaliyofanyika katika viwanja vya Malamala kata ya Igoma mkoani Mwanza.

Maonesho hayo yamefunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel.

Akiwa katika banda la  Wizara ya Viwanda na Biashara, Mkuu wa Mkoa, Robert Gabriel, amesisitiza kutumia muda huu wa maonesho kutoa elimu zaidi kwa vijana wazawa, ili kuwajengea morali ya uzalendo itakayolisaidia taifa siku za usoni.

Aidha, Robert Gabriel ameishukuru Wizara ya Viwanda na Biashara kwa  ushiriki wake katika matamasha na maonesho mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika hapa nchini

"Wizara imekuwa ikishiriki na kutoa elimu kwa wajasiriamali wetu hapa nchini, na kuwajengea uelewa mkubwa wa kufanya Biashara katika  mazingira mbalimbali katika nchi yetu,” amesema RC Gabriel.

Nae Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Richard Pweleza,  akiongea na  wanafunzi  kutoka  Shule ya Sekondari  Shamaliwa, amewaeleza  kuhusu  majukumu mbalimbali  yanayofanywa na wizara hiyo na kuwapa  elimu kuhusu dhana ya KAIZEN na namna ya kuitekeleza.

Pweleza amewataka  kutumia KAIZEN na kuiweka  katika  mfumo bora wa kujisomea, utakaowawezesha kusimama katika mazingira safi na salama yatakayo wasaidia kuwa wawekezaji wazuri, pindi muda utakapofika kwa wao kulihudumia taifa.

Maonesho hayo ni mwendelezo wa shamrashamra za kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru, ambayo yameanza Novemba 23 na yanatarajiwa kufikia kilele Disemba 2 mwaka huu, yakibebwa na kauli mbiu isemayo "MAWASILIANO NI MSINGI WA UCHUMI, JE UMEWASILIANA"

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c071186817658edf518bb7c32b6b97b2.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Anthon Chuwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi