loader
TPSF: Ubia njia sahihi kufaidi fursa bomba la mafuta EACOP

TPSF: Ubia njia sahihi kufaidi fursa bomba la mafuta EACOP

MKURUGENZI  Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Tanzania (TPSF) Francis Nanai ameshauri kampuni za Kitanzania na Uganda kuunganisha nguvu kupitia ubia ili kukidhi sifa za kupata kandarasi na zabuni mbalimbali kutoka kwenye mradi wa bomba la mafuta linaloanzia Kabaale-Hoima hadi Chongoleani, Tanga.

Akizungumza katika kongamano la mafuta na Gesi na Mafuta lililowaleta pamoja wadau wa sekta hiyo kutoka Uganda na Tanzania leo Jumamosi, jijini Dar es Salaam, Nanai amesema utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta (EACOP) unaoanzia Hoima, Uganda hadi Tanga ni fursa inayohitaji ushirikiano wa pamoja baina ya kampuni ili kuweza kufaidi matunda yake.

Kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.5 zinatarajiwa kuwekezwa moja kwa moja kwenye mradi huo urefu wa km 1,443 wakati kiasi kingine zaidi ya dola za Marekani bilioni 20 zitatumika kwenye mnyororo wa miradi midogomidogo inayotokana na EACOP.

“Hii ni fursa kubwa kwa Waganda na Watanzania kupitia ubia na ushirikiano na kufaidi biashara hii kubwa,” amesema Mkurugenzi huo.

Mkuu huyo wa TPSF amesisitiza mbele wa wadau hao wa sekta ya mafuta na gesi kuwa sekta binafsi kutoka Uganda na Tanzania zinahitaji ‘msuli wa kifedha’ ili kuweza kutoa huduma mbalimbali kupitia mradi huo.

“Hapa kampuni kuungana na ubia unapohitajika kuhamasishwa miongoni mwa watu wa mataifa haya mawili,” ameongeza.

Akitaja sifa nyingine zinazohitajika ili kufaidi matunda ya mradi huo mkubwa Afrika Mashariki, Nanai alisema wadau wanapaswa kuwa na taaluma, ujuzi na uzoezu katika nyanja tofauti tofauti ili kuweza kuvuna “rasilimali hizi zilizotolewa na Mungu.

Naye Mgeni rasmi katia kongamano hilo la siku mbili, Waziri wa Waziri wa Nishati, January Makamba amewaasa wananchi wa Uganda na Tanzania kushirikiana na kwa kuunganisha nguvu ili kupata fursa za mradi huo ambao umeanza kutekelezwa katika hatua za mwanzo.

Akizindua kongamano hilo jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi, Makamba amesema: “Zipo fursa nyingi zitokanazo na mradi  wa bomba kutoka Kaabale Uganda hadi Tanga…. kufanikiwa katika fursa hizo lazima mshirikiane kwa pamoja kiasi kwamba Watanzania wana uwezo wakuwekeza Uganda,” alisema.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/fd9c1550f4df335ccf496076115325f3.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi