loader
Watanzania, Waganda watakiwa kushirikiana fursa bomba la mafuta

Watanzania, Waganda watakiwa kushirikiana fursa bomba la mafuta

WATANZANIA na Waganda wametakiwa kushirikiana kuzitumia fursa zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) ambapo hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo zimeanza.

Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa Nishati, January Makamba alipokuwa akizindua kongamano la mafuta na gesi linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC). “Zipo fursa nyingi zitokanazo na mradi wa bomba kutoka Uganda hadi Tanga, Tanzania lakini ili kufanikiwa kuzitumia fursa hizo lazima mshirikiane kwa pamoja kiasi kwamba Watanzania wawe na uwezo wakuwekeza Uganda ambako mradi unapita na Waganda vivyo hivyo kulingana na uhitaji wa maeneo husika,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Francis Nanai alisema kongamano hilo la siku mbili linalofikia kilele leo na kuhudhuriwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni pamoja na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan litatoa mwanga na mwelekeo wa ushirikiano baina ya sekta binafsi ya Tanzania (TPSF) na ya Uganda (PSFU).

“Tupo hapa leo kwa ajili ya kupeana uzoefu na kutengeneza mazingira rafiki yatakayorahisisha sekta binafsi ya Uganda na Tanzania kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi wa EACOP ambao una fursa nyingi,” alisema.

Nanai aliainisha baadhi ya fursa ambazo sekta binafsi inaweza kutekeleza kuwa ni usafirishaji, kampuni za ulinzi, huduma ya chakula na vinywaji, hoteli na nyumba za kulala wageni, rasilimali watu, vifaa vya ujenzi, vifaa vya kiofisi, kazi za kiuhandisi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Aidha, Nanai alisema kuwa lengo la kongamano hilo nikuwapa wigo mpana wafanyabiashara ili waweze kujua faida na changamoto tarajiwazo katika mradi huo ambapo wameangazia zaidi katika sheria za nchi zote mbili na sera zinazoshabihiana na sekta ya ujenzi, hususani bomba la mafuta.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/5a7a064f016ea4a122221ff00c43932b.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Dunstan Mhilu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi