loader
Taasisi ya Mifupa Muhimbili kushirikiana na madaktari wa China

Taasisi ya Mifupa Muhimbili kushirikiana na madaktari wa China

TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesaini mkataba wa ushirikiano na Chama cha Madaktari China (CMA) pamoja na Hospitali ya Tian Tan kwa lengo la kuboresha huduma za kibingwa hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.

“Mkataba huo wa ushirikiano una manufaa makubwa upande wa gharama za vifaa tiba, kwani China ina viwanda vingi hivyo itasaidia MOI kupata vifaa tiba kwa bei nafuu na kupelekea gharama za matibabu kushuka,” alisema.

Akifafanua zaidi, Dk Boniface alisema kuwa faida nyingine za mkataba huo ni kuimarisha ushirikiano baina ya MOI na CMA kwa kuwezesha wataalamu kutoka China kuja kutoa huduma nchini Tanzania na wataalamu wa Tanzania kupata fursa ya kwenda kujifunza nchini China.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki alisema hatua ya MOI kuingia mkataba huo na CMA pamoja na Hospitali ya Tian Tan italeta mapinduzi makubwa kwenye utoaji wa huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu nchini Tanzania

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/52e6767aeed0a8e42b39fcaf09ac7139.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi