loader
Wanafunzi wa kike SUA waibuka vinara

Wanafunzi wa kike SUA waibuka vinara

WANAFUNZI wa kike katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), wamekuwa vinara kwa kuongoza kwenye ufaulu wa masomo na kuzoa zaidi ya asilimia 60 ya zawadi zilizotolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri kipindi cha mwaka huu.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Shahada za Awali SUA, Dk Nyambilila Amour, alisema hayo katika taarifa yake kwenye hafla ya utoaji zawadi na kuwatambua wanafunzi mbalimbali waliofanya vizuri katika masomo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Nyambilila alisema mwaka huu wanafunzi wa kike wameongoza kutokana na kujitahidi kwa kiasi kikubwa kutekeleza sera za chuo na uzingatiaji wa usawa wa kijinsia na kufanya ongezeko la zaidi ya asilimia 60 ya zawadi zilizotolewa kunyakuliwa na wanafunzi hao. “Uwiano wa ufaulu kwa mwaka huu kati ya waliopewa zawadi zaidi ya asilimia 60 ni watoto wa kike na asilimia 40 ni wa kiume.

Hii inatoa faraja hasa tunapozungumzia usawa wa kijinsia, kwamba wakifundishwa wote kwa pamoja basi wanaweza kufikia malengo tarajiwa,” alisema Nyambilila. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Raphael Chibunda, alisema kuwa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo kwa wanafunzi na wafanyakazi hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutambua na kuwaenzi wanafunzi waliofanya vyema kwenye taaluma.

Chibunda alisema jumla ya tuzo 2,020 zimetolewa katika vipengele mbalimbali ikiwemo wanafunzi bora 202, tuzo tano za utafiti, tuzo tano za uongozi pamoja na tuzo sita za ukurasa wa mtandao bora wa idara za chuo kikuu hicho. Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji Mali Mkoa wa Morogoro, Dk Rozaria Rwegasila kwa niaba ya Katibu Tawala wa mkoa huo alikishauri chuo kikuu hicho kuwa na utamaduni wa kukagua mara kwa mara vigezo vya kuchagua wanafunzi na watafiti bora kitaaluma.

Rozaria alisema kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kutasaidia kwa kiasi kikubwa ukuzaji wa ujuzi pamoja na uvumbuzi na ubunifu wa kisayansi, hivyo itasaidia taifa kupiga hatua kiuchumi na kisayansi.

Pamoja na hayo aliuomba uongozi wa chuo hicho kuangalia namna ya kuongeza kiwango cha utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi ikiwemo kutoa ufadhili wa mosomo kwa mwaka mmoja. “Nikipongeze chuo kikuu hiki kwa kuwatambua wanafunzi hawa na inapowezekana mzingatie hata utoaji ufadhili wa masomo kwa wanafunzi bora kila mwaka,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/9aa62d6de2bd42b4ff12a1594bd9c0aa.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi