loader
Wanawake tutumie siku 16 za kupinga ukatili kupata ufumbuzi

Wanawake tutumie siku 16 za kupinga ukatili kupata ufumbuzi

WIKI iliyopita umefanyika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wenye kauli mbiu mwaka huu isemayo” Komesha ukatili wa kijinsia sasa.”

Siku hizo zinaadhimisho ulimwenguni kote na maadhimisho yalianza Novemba 2 mwaka huu na yatakamilika Desemba 10 mwaka huu na katika siku hizo masuala mbalimbali yatafanyika kwa lengo la kupambana na vitendo hivyo lakini pia ni wakati muafaka wa kutafakari juu ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Ndani ya siku hizo jamii ina haki na wajibu wa kuhoji ubaguzi na kuunga mkono usawa wa kijinsia katika mtazamo wa kijinsia, lakini kila mtu ana jukumu la kuzuia ukatili unaofanyika kwenye familia, watu binafsi, shule, mahali pa kazi, nyumba za ibada, vilabu vya michezo na serikali.

Ikiwa wewe au mtu unayejua, amefanyiwa ukatili wa kijinsia, unaweza kufika katika vyombo husika vinavyotoa msaada wa Kisheria, unga mkono usawa wa kijinsia, heshimu na usiwe sehemu ya ukatili na vaa nguo zenye rangi ya chungwa kuonesha ishara ya amani katika kipindi cha kampeni.

Inaelezwa kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza kila mmoja kutafakari na kuwa tayari wakati wote kupinga vitendo vya ukatili na kutafuta njia za kuwasaidia waathirika wa ukatili.

Pia kuchukua hatua kwa kuingilia kati kwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili na kuhusisha wadau wa maendeleo, azaki, na jamii katika kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia. Rangi ya chungwa ni rangi iliyochaguliwa na Umoja wa Mataifa na inawakilisha mustakabali huru na hatimaye baadaye isiyo na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Watu wanashauriwa kuvaa fulana au mashati ya rangi ya chungwa ili kuunga mkono na kumaliza ukatili katika familia na kushawishi serikali na vyombovya maamuzi kuharakisha mapitio ya maboresho ya sera na sheria kandamizi zinazochochea ukatili wa kijinsia ili kufikia malengo yaliyowekwa katika Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Katika maadhimisho haya ni vema wanawake wakujitokeza kwa wingi katika kushiriki katika matukio mbalimbali ili kuonesha mchango wa wanawake katika kupiga ukatili huo wa kijinsia na kuhakikisha elimu inapatikana kwa wanawake wote ndani ya siku hizi.

Katika miaka ya karibuni ,tumeshuhudia vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiongezeka dhidi ya wanawake ikiwemo vipigo, kubakwa na kubwa zaidi ni kuuawa kwa wanawake kwa njia mbalimbali hivyo ni wakati wa kutafakari kwa kina.

Ndani ya siku hizo yatafanyika matukio mbalimbali ambayo yatasaidia kupunguza ukatili wa kijinsia hivyo, ni vema kupitia matukio hayo yapatikane matunda na matokeo chanya yaonekane. Kama ilivyofanyika wakati wa uzinduzi wa siku hizo ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizindua mwongozo wa uanzishwaji ,uendelezaji na ufuatiliaji wa dawati la jinsia katika taasisi za elimu ya juu na kati lakini pia akataka yaanzishwe madawati ya jinsia katika shule za sekondari na msingi.

Hili la madawati ni dhahiri kuwa litasaidia kwenye kukomesha ukatili mashuleni iwapo yatatumika vizuri kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike na hivyo kupunguza ukatili kwao lakini pia waweze kukabiliana na ukatili katika maeneo ya shule. Lakini ni vema kuhakikisha katika ngazi za familia na pengineko inatafutwa suluhu ya kudumu ya kukabiliana na ukatili unaotokana na mila na desturi na masuala mengine na kuhakikisha yanafanya kazi ili kukomesha ukatili huo.

Lakini pia ni vema ndani ya siku hizo 16 jamii ijipime na kuangalia namna bora ya kukabiliana na vitendo hivyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/9b7555a52199759aa8ad61310f01a08d.jpeg

KATIKA ukurasa wake wa habari za kimataifa ...

foto
Mwandishi: Na Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi