loader
Dk Mwinyi: Tumieni msikiti kujadili matatizo ya jamii

Dk Mwinyi: Tumieni msikiti kujadili matatizo ya jamii

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewataka waumini wa dini ya Kiislamu katika Shehiya ya Unguja Ukuu, kutumia vyema msikiti wa Al-Noor kwa kujadili matatizo yanayoihusu jamii na kuyatafutia ufumbuzi.

Alitoa rai hiyo kwa waumini wa shehia hiyo na vitongoji vya jirani wakati alipozungumza nao katika ufunguzi wa Msikiti wa Ijumaa wa Al-Noor baada ya kukamilika ujenzi wake, tukio lililokwenda sambamba na ibada ya sala ya Ijumaa juzi. Alisema kuna umuhimu waumini kutumia vikao vya misikiti kujadili masuala mbalimbali pamoja na changamoto zinazohusu jamii ikiwemo yatima, wajane pamoja na wenye ulemavu ili kuzipatia ufumbuzi.

Aliwaeleza waumini hao kwamba kama walivyofanikiwa kuanza kwa mafanikio ujenzi wa msikiti huo na kufikia hatua ya kuridhisha, ndivyo wanaweza kukaa pamoja na kujadili changamoto na maovu yanayoihusu jamii, ikiwemo suala la udhalilishaji kijinsia ambalo alisema limekithiri.

Dk Mwinyi alisema mapambano dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia sambamba na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ni jambo linalohitaji nguvu ya jamii na si suala linaloihusu serikali pekee. Naibu Kadhi kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Shehe Mahamoud Mussa Wadi aliwataka waumini kuepuka mifarakano, kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza pamoja na kudumisha usafi wa msikiti.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/61b16b8aef46d667858239f5d039a320.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi