loader
Wakulima waomba mfumo utambuzi mbegu asili

Wakulima waomba mfumo utambuzi mbegu asili

WAKULIMA wameiomba serikali kuweka mfumo wa utambuzi wa mbegu za asili ili kurudisha vyakula vya asili na kuepukana na madhara mbalimbali yanayotokana na upungufu wa mlo kamili na lishe. Ombi hilo lilitolewa wilayani Karatu, mkoani Arusha wakati wa majadiliano ya mfumo wa mbegu katika maonesho ya mbegu za asili na vyakula yaliyofanyika Viwanja vya Mazingira Bora.

Mmoja wa wakulima, Ansila Pascal kutoka Kijiji cha Rotiya aliiomba serikali kuweka kipaumbele kwenye mbegu ziweze kujulikana na kutambulika na pia wakulima kujali asili yao ili mbegu kuwa na ubora kuliko mbegu za kisasa. K

wa upande wake, Elibaraka Joseph kutoka Kata ya Mbulumbulu aliomba vikundi vya wakulima kuendelea kuhamasisha mbegu za asili pamoja na taasisi za kitafiti kupata nguvu ya fedha ili ziendelee kutoa elimu za namna gani ya kutunza mimea ya vinasaba hapa nchini.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazao na Kilimo, Beatus Malema alisema lengo la kuwakutanisha wakulima ni kuunda jukwaa la wakulima na mbegu za asili kwa kujenga hamasa juu ya umuhimu wa kutumia vyakula na mbegu za asili kwa faida ya afya na kipato kwa wananchi. Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Abas Kayanda alisema maonesho ya wakulima yawe yanatumika kama mashamba darasa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia vyakula na mbegu za asili.

Alitoa rai kwa wananchi kutotupa mbegu za maboga kwa kuwa zinaweza kutumika kama lishe na dawa. Aliwataka wafahamu umuhimu wa mbegu kwa kuwa zina faida kimapato na kimwili na kuziweka kwenye maduka ya pembejeo kwa kuwa hazina gharama yoyote.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na Wafugaji Mkoa wa Arusha (Mviwa Arusha), John Safari alisema wakulima wana mchango mkubwa kwa usalama wa chakula na kutumia mbinu za teknolojia mpya za chakula. Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira alisema iko haja ya kutumia mbegu za asili kibaiolojia zidumu na kuziendeleza ikiwa ni pamoja na kujua umuhimu wa kuwa na sheria mahususi kwa ajili

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/3370e0e8df986f0633546a768b190ee8.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Veronica Mheta, Karatu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi