loader
Mil 311/- zanufaisha vikundi 78

Mil 311/- zanufaisha vikundi 78

MKOA wa Mara umetumia Sh milioni 311.19 kuchangia mfuko wa wanawake, vijana na wenye ulemavu katika mwaka wa fedha 2021/2022 mpaka kufi kia Septemba, mwaka huu na kunufaisha jumla ya vikundi 78.

Taarifa hiyo iliwasilishwa kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa jana na kujadiliwa chini ya Mwenyekiti ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi.

Ilisema kiasi hicho ni sawa na asilimia 68 ya fedha iliyopaswa kutolewa kwenye Sh bilioni 4.59 ambayo ni mapato halisi ya halmashauri zote katika kipindi hicho. Wakati halmashauri mbili zimechangia mfuko huo kwa zaidi ya asilimia 100, nyingine mbili hazikuchangia na tano zilichangia kwa viwango tofauti.

Halmashauri ya Serengeti imechangia jumla ya Sh 43,300,520 sawa na asilimia 169 wakati Halmashauri ya Bunda ikiwa imechangia jumla ya Sh milioni 22 sawa na asilimia 110. Tarime imechangia jumla ya Sh 174,169739 sawa na asilimia 77 huku Manispaa ya Musoma ikiwa imechangia Sh 38,400,000 sawa na asilimia 72 kama ilivyo kwa Halmashauri ya Butiama ambayo ilichangia jumla ya Sh 17,111,285.

Halmashauri ya Musoma ilichangia Sh 11,706,108 sawa na asilimia 36, Rorya Sh milioni 1.5 sawa na asilimia saba huku Miji ya Bunda na Tarime ikiwa haijachangia kiasi chochote. Ilielezwa kwamba, kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 halmashauri zote za mkoa huo zilitumia jumla ya Sh bilioni 1.26 sawa na asilimia 90 ya fedha zilizopaswa kutolewa kwenye makusanyo halisi ya ndani kuchangia mfuko wa vikundi hivyo.

Hapi aliagiza wakurugenzi wa halmashauri zote ambazo hazikufikisha asilimia 100 katika kuchangia mfuko huo katika mwaka wa fedha 2020/2021 kujieleza kwa maandishi ili ufumbuzi upatikane katika kutekeleza mpango huo wa taifa wenye lengo la kuwezesha wananchi kiuchumi

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/bcb9a2779f6fe64139cf9eb42616fb48.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Editha Majura, Musoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi