loader
Morrison arudisha furaha Simba SC

Morrison arudisha furaha Simba SC

MABAO mawili ya kiungo mshambuliaji Benard Morrison na moja la Meddie Kagere yameipa Simba ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Red Arrows ya Zambia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jana.

Katika mechi hiyo ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba ilipata mabao hayo katika dakika ya 16, mfungaji akiwa Morrison kwa mpira wa adhabu huku Kagere akiongeza bao la pili katika dakika ya 19 akimalizia pasi ya raia huyo wa Ghana.

Morrison aliyekuwa katika kiwango bora jana, aliihakikishia timu yake ushindi baada ya kufunga bao la tatu katika dakika ya 77, akimalizia kwa shuti mpira wa kurushwa wa Mohammed Hussein. Mchezo huo uliokuwa na presha kwa wageni katika dakika ya 29, Simba ilipata penalti baada ya Hassan Dilunga, kuangushwa ndani ya boksi na Nickson Mubili lakini Morisson, alishindwa kufunga baada ya kipa Charles Kalumba kuiokoatimu yake kwa kupangua mkwaju huo.

Red Arrows walinza kwa kasi kipindi cha pili na kupata kona katika ya dakika 46 baada ya Morrison kuuzuia mpira wa James Chamanga, wakati huo huo kocha Pablo Martin alifanya mabadiliko kwa kumtoa Paschal Wawa na nafasi yake kuchukuliwa na Henoc Inonga. Dakika ya 57, Red Arrows walipata pigo baada ya beki wake wa kushoto Prosper Chiluya kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi kiungo mshambulia wa Simba Dilunga.

Katika dakika ya 72 Simba, almanusra waandike bao baada ya Morrison, kupiga shuti kali la mita 18 ambalo liliokolewa na kipa Kalumba na kuwa kona. Kocha wa Simba Pablo Martin, katika dakika ya 73 alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Dilunga na Sadio Kanoute huku nafasi zao zikichukuliwa na Ibrahim Ajib na Mzamiru Yasin ili kuimarisha zaidi safu ya kiungo ya timu yake.

Simba ilifanya mabadiliko mengine katika dakika ya 79 kwa kumtoa Kagere na nafasi yake kuchukuliwa na nahodha John Bocco. Matokeo hayo yanaipa faida Simba katika mechi ya marudiano Desemba 5 nchini Zambia, kwani sasa wanahitaji kulinda mabao yao ili kusonge mbele hatua ya makundi

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f1ee7dac524150c25d84467871a45af8.jpeg

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania ...

foto
Mwandishi: Na Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi