loader
TBS yajivunia ushiriki Shimmuta

TBS yajivunia ushiriki Shimmuta

WACHEZAJI wa timu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wamejivunia mafanikio waliyoyapata kwenye michezo ya Shirikisho la Mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) yaliyomalizika Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizunguza na waandishi wa habari mkoani hapa juzi, Katibu wa Michezo wa TBS, Nyabuchwenza Methusela imekuwa fursa nzuri kwao kuwa pamoja na wenzao wa mashirika mengine. Alisema wao kama TBS wameshirika michuano hiyo na wamepata manufaa mengi ikiwa ni pamoja na kujenga urafiki, kufahamiana, lakini pia inatangaza mashirika yao.

“Kuna mashirika mengi ya umma na binafsi hapa nchini, lakini wakati mwingine kuyafahamu inakuwa vigumu, lakini kupitia michezo tunafahamiana na mashirika hayo ikiwa ni pamoja na kujua yanajishughulisha na nini,”alisema Methusela. “Lakini michezo inakulazimisha kufanya mazoezi kwa sababu unajua una mashindano.

Kukulazimisha huko moja kwa moja kunakujengea afya ya mwili na akili, ambapo utaweza kufanyakazi zako vizuri, lakini pia itakuepusha na magonjwa mbalimbali hasa yale yasiyoambukiza,” alisema, Methusela. Alitoa mwito kwa Serikali kuweka nguvu kwenye mashindano hayo.

Katika michuano hiyo, michezo ambayo TBS ilifanya vizuri ni netiboli ambapo waliwabwaga Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa mabao 38-28, wakaitandika Benki Kuu Tanzania (BoT) kwa mabao 52-12 na kisha kuibuka na ushindi wa magoli 40-12 dhidi ya Mwalimu Nyerere.

Ushindi mwingine kwenye mchezo huo ni wa mabao 28-15 dhidi ya Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU). TBS ilifanya vizuri pia kwenye Soka, Wavu, kuvuta kamba na kurusha vishale. Mashindano ya SHIMMUTA yalianza Novemba 13, mwaka huu na kumalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8a502b4be9b5d31998c376bf47b1c530.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi