loader
Chid Benz kuachia albamu kesho

Chid Benz kuachia albamu kesho

MKONGWE wa muziki wa Bongofl eva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ (pichani), amesema kuwa baada ya kukamilika kila kitu kesho anaiachia albamu yake ya ‘Watu wangu’, ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.

Katika albamu hiyo ambayo ina nyimbo 18, Chid Benz, amewashirikisha wasanii wanne wote kutoka hapa nchini ambao ni Baddest, Only 1 Pablo, Scar Mkadinali na Brian Simba.

Watu wangu imebeba nyimbo kama Intro, King of the Jungle, Walete, Simuoni, Hilo Ngoma, Nalia, Dreams, Jirani, Noumer, Nahamia Bar, Wapi Utakwenda, One, Mapito, Supastar, Step by Step,Nikisema, Mama na Zoom.

Akizungumza na gazeti hili jana,Chid Benz alisema kuwa huu ni wakati wa mashabiki kupata ladha ya muziki mzuri kutoka kwake kwani albamu ya ‘Watu Wangu’ imeandaliwa na watayarishaji wenye viwango vya hali ya juu.

“Baada ya mashabiki wangu kuisubiri kazi hii kwa muda mrefu sasa huu ni wakati wao wa kufurahia ladha halisi ya muziki wa bongofleva ambayo ilipotea kwa muda sasa imerudi rasmi nawaomba waipokee ‘Watu Wangu’,” alisema Chid Benz.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6d1766bed5df6429fc333ed113d22ff2.jpeg

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi