loader
Watoto watumikishwa kwa ujira wa chakula

Watoto watumikishwa kwa ujira wa chakula

BAADHI ya wakazi wa Wilaya ya Maswa wameitaka serikali na wadau wengine kutilia mkazo zuio la ajira kwa watoto ili kuwawezesha kwenda shule na kutekeleza ndoto zao.

Aidha imeelezwa kuwa wengi wa watoto hao hasa upande wa mama lishe hutumikishwa kwa ujira wa chakula. Wanasema kwa sasa watoto wameonekana wakifanya biashara ndogo ndogo hali inayowafanya kukosa masomo pamoja na haki zao zingine za msingi. Wananchi hao katika mahojiano wamesema kwamba ajira kwa watoto zinaoneka kukithiri, hasa katika stendi za mabasi na magulio. Juma Saidi aliliambia Gazeti hili kwamba wengi wa watoto hao ni wenye umri wa kwenda shule lakini wanaajiriwa kufanya biashara ndogo ndogo kwa ujira ndogo wa Sh 1,000 hadi Sh2,000 kwa siku.

“Tatizo ni kwamba ajira hizi zinawaingiza katika mazingira hatarishi,,” alisema. Kwa mujibu wa Said, mama lishe ni miongoni mwa makundi yanayowatumikisha watoto , hasa kutokana na ukweli kwamba hawana uwezo wa kujitetea kimaslahi, hivyo kupokea kiasi chochote cha ujira.

Mkazi mwingine Gift Clement, alisema wakati mwingine watoto hao hawalipwi chochote zaidi ya kupewa chakula na wamekuwa wakitumikishwa hata kwa kazi za ndani. “Hali ni mbaya zaidi kwa watoto wa kike ambao wanakua katika mazingira hatarishi zaidi, ikiwemo mimba za utotoni na ukatili wa kingono kwa ujumla,” alisema.

HabariLeo ilikutana pia na watoto hao (majina yamehifadhiwa) ambao wengi wao wana umri kati ya miaka 8 na 10, wakikiri kulipwa ujira mdogo ili waweze kujikimu. Takribani wote walieleza jinsi wanavyofanyishwa kazi kwa muda mrefu bila kulipwa isipokuwa kupewa chakula na nauli.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge alisema tayari ameiagiza idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Ofisa ustawi wa jamii wilayani humo kuhakikisha suala hilo linakomeshwa. “Ni kweli tatizo lipo na wahusika wote wanaotumikisha watoto watachukuliwa hatua za kisheria,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/7e657b2477eba50a1548ae58b6ce9fb4.jpeg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Na Happy Mollel, Simiyu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi