loader
Upandaji miti unazuia mabadiliko ya tabia nchi

Upandaji miti unazuia mabadiliko ya tabia nchi

KAMPUNI ya Qnet imezindua mradi wa upandaji miti uitwao ‘Urithi wa Kijani.’

Kupitia mradi huo, shirika hilo limepanda zaidi ya miti 3000 barani Afrika na Asia.

Nchini Kenya, mradi huo unafanywa katika maeneo ya vijijini chini ya ushirikiano na kikundi kiitwacho Trees4Kenya.

Akizungumza nchini Kenya mara baada ya ziara yake eneo la Embu, ambako litatekeleza upandaji mti, mratibu wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Qnet, Muqtadir Suwani, amesema kwa kushirikiana na Trees4Kenya, wanajitahidi kubadilisha kiwango cha kaboni cha Kenya na kwamba lengo ni kujenga jumuiya endelevu kote barani Afrika.

Amesema hakuna wakati kama wa sasa wa kuwa rafiki na mazingira na kwamba Qnet inaunga mkono jitihada za serikali kutunza mazingira na kuleta mabadiliko chanya.

Suwani amesema mradi huo ni ushirikiano wa wadau mbalimbali unaofanya kazi katika ngazi ya jamii kupitia ushirikiano na wadau kama vile EcoMatcher na kikundi cha Trees4Kenya.

Naye Mkurugenzi wa Trees4 Kenya, Paulino Mugendi amesema ushirikiano wa sekta binafsi ni muhimu ili kuokoa misitu ya Kenya.

“Tunashukuru sana Qnet na washirika wao kwa msaada huu, ni kwa kupanda miti tu ndipo tunaweza kulinda mazingira yetu vyema,” amesema mwanamazingira huyo.

Amesema tayari wamepanda mamia ya miti na kupitia mradi huo wanatarajia kupanda zaidi ya miti 1000 na kwa njia hiyo kusaidia kurejesha misitu nchini Kenya.

Kwa upande wa Mtaalamu wa Misitu kutoka Forestry Kenya, Karuku Kathogo, amesema ili kulinda mazingira, kupanda miti pia kunasaidia maendeleo endelevu ya jamii.

Mipango hii inahakikisha kwamba tunakuwa na jumuiya endelevu ambayo haiharibu mazingira yake kwa jina la maendeleo; amesema

Akinukuu maneno ya marehemu Wangari Mathai, mwanzilishi wa Green Belt Movement nchini Kenya ambaye aliwahi kusema, “watu maskini watakata mti wa mwisho ili kupika mlo wa mwisho.”

Mwanamazingira alisema maneno hayo akimaanisha jitihada za utunzaji mazingira lazima ziende ana kwa ana na utokomezaji wa umaskini.

Mathai alihamasisha upandaji wa zaidi ya miti milioni 30, na kuhamasisha Umoja wa Mataifa kuanzisha kampeni ambayo imesababisha kupanda miti bilioni 11duniani kote.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d1ef7e02f826f24f24c5e4a615bb56ff.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi