loader
Mwandishi asimamishwa kazi kwa kumsaidia kaka yake

Mwandishi asimamishwa kazi kwa kumsaidia kaka yake

MTANGAZAJI mashuhuri wa CNN Chris Cuomo amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana baada ya kuibuka maelezo mapya kuhusu juhudi zake za kumsaidia kaka yake, Andrew M. Cuomo, gavana wa zamani wa New York, alipokuwa akikabiliwa na msururu wa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia zilizosababisha kiongozi huyo kujiuzulu.

Awali Chris Cuomo aliomba radhi kwa kuwashauri wasaidizi wakuu wa kisiasa wa Andrew Cuomo - jambo ambalo ni ukiukaji wa utamaduni wa jadi kati ya waandishi wa habari na wabunge.

Maelfu ya kurasa za ushahidi uliotolewa Jumatatu na Mwanasheria Mkuu wa New York, Letitia James, ulifichua kuwa jukumu la Chris lilikuwa zaidi kuliko ilivyojulikana hapo awali.

"Hati hizo, ambazo hatukuwa tumezijua kabla ya kutolewa kwa umma, zinazua maswali mazito," CNN ilisema katika taarifa Jumanne. "Chris alipokiri kwetu kwamba alikuwa ametoa ushauri kwa wafanyikazi wa kaka yake, alivunja sheria zetu na tulikubali hilo hadharani. Lakini pia tulithamini nafasi ya kipekee aliyokuwa nayo na tulielewa hitaji lake la kuweka familia kwanza na kazi ya pili. Hata hivyo, hati hizi zinaonyesha kiwango kikubwa cha kuhusika katika jitihada za ndugu yake kuliko tulivyojua hapo awali.

"Kutokana na hilo, tumemsimamisha kazi Chris kwa muda usiojulikana, tukisubiri tathmini zaidi," mtandao huo uliongeza.

Ushirika wa Chris katika kipindi cha miezi 18 iliyopita ya ugavana wa kaka yake kumeiumiza zaidi CNN, ambayo ilisimama karibu na mtangazaji wake wa hali ya juu hata nakuleta maswali juu ya kusimamia misingi ya mtandao huo na viwango vya uandishi wa habari.

Jeff Zucker, Rais wa CNN, alimuunga mkono Bw. Cuomo kwa miezi kadhaa, akisita kumwadhibu hata baada ya ripoti kuonyesha kwamba mtangazaji huyo alishiriki katika vikao vya mkakati na timu ya kisiasa ya kaka yake.

Mapema mwaka huu, mtandao huo ulipendekeza wazo kwa Bw. Cuomo kwamba anaweza kuchukua likizo ya muda ikiwa angetaka kuzingatia rasmi kusaidia utetezi wa kaka yake.

Katika barua pepe nyingi na ujumbe mfupi kati ya watu wa karibu wa kaka yake Cuomo, alitoa ushauri mara kwa mara - "Tafadhali niruhusu nisaidie kwa maandalizi," alimtumia msaidizi mkuu mwezi Machi - na akafanya jitihada za kufuatilia hali ya makala zinazosubiri kutoka katika vyombo vingine vya habari, vikiwemo Politico na The New Yorker, zikuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono na Andrew Cuomo.

Wakati mmoja, msaidizi mkuu wa zamani wa gavana, Melissa DeRosa, alimuliza mtangazaji kama angeweza kuangalia "vyanzo" vyake kuhusu uvumi kwamba mtandao wa Politico ilikuwa ikifanya kazi mashtaka ya ziada ya kaka yake na Chris alijibu “Naiangalia.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/73afe773c41c0538173c9301ec1a1aa6.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: CNN

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi