loader
Wizara ya Viwanda yajipanga kutoa tuzo kwa wanafunzi wabunifu

Wizara ya Viwanda yajipanga kutoa tuzo kwa wanafunzi wabunifu

WIZARA ya Viwanda na Biashara imepanga kutoa tuzo kwa mwanafunzi atakayebuni na kutengeneza kifaa, mfumo ama nyenzo inacyoweza kutatua changamoto za kijamii na taifa.

Waziri wa wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo alisema hayo wakati akikabidhi tuzo na zawadi kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wanaohitimu ili kuwahamasisha waliobaki kufanya vizuri zaidi ikiwa na kuonyesha ubunifu wao.

Profesa Mkumbo alisema tuzo hiyo itaanza kutolewa kuanzia mwaka kesho na wizara hiyo kwa waziri yeyote atakayekuwepo.

Alisisitza kuwa tuzo hiyo ya wizara itakayotolewa itachochea ubunifu kwa wanafunzi na kuhamasisha watendaji wa viwanda kuwafuata kwenye taasisi hiyo kwa kuwa katika suala la viwanda taasisi hiyo ina uwezo mkubwa wa kutoa wanafunzi wenye uwezo wa kufanya kazi.

“Dira yetu ni kwamba ikifika mwaka 2025 umaskini Tanzania uwe ni historia, chuo kina nafasi ya pekee ya kuchangia kwenye huo mwelekeo.

“Walimu mzingatie mwelekeo mpana wa mambo ya kisera,  rasilimali tunazo tunahitaji vijana mchangamshe bongo zenu ili tupate bidhaa, mtengeneze fedha nchi ipate mapato,” alisema.

Naye Mkuu wa DIT, Profesa Preksedis Ndomba alisema taasisi hiyo inatoa tuzo katika kila programu kila mwaka ili kujenga ushindani na kuhamasisha juhudi kwa kila mwanafunzi.

Alisema tuzo zinazotolewa katika makundi mbalimbali ni cheti na fedha.

Mwenyekiti wa Baraza katika chuo hicho, Dk Richard Masika aliwataka wanafunzi hao kutumia akili, maarifa, ujuzi na uwezo walionao ili kubuni vitu mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Energy Plus ambaye ni mhitimu wa miaka ya nyuma katika taasisi hiyo aliwataka wahitimu kutumia muda vizuri ili kuchochea maendeleo tofauti na hapo nafasi mbalimbali za juu katika viwanda zitakuwa zinachukuliwa na waajiriwa kutoka nchi jirani.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/67015c01eb1a320b86591cd7ded14fa1.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi