loader
Tanzania yafuzu Kombe la Dunia

Tanzania yafuzu Kombe la Dunia

TIMU ya taifa ya soka la watu wenye ulemavu ya Tanzania, Tembo Warriors, imekuwa ya kwanza kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Uturuki.

Mbali na kufuzu kwa fainali hizo, pia timu hiyo imekuwa ya kwanza kutinga nusu fainali ya baada ya jana kuichapa bila huruma Cameroon kwa mabao 5-0 katika robo fainali ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (Canaf 2021) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezwa kuanzia saa 2:00 asubuhi, Tembo walionesha mchezo mzuri na wa kuvutia, huku wakipiga pasi moja moja katika staili ya mstatili na kuwapoteza Cameroon walionekana wenye miili iliyojengeka na warefu kuliko Tembo Warriors.

Mpaka wanakwenda mapumziko, Tembo Warriors walikuwa wanaongoza kwa mabao 3-0 na kipindi cha pili wakaongeza mabao 2-0 na kuibuka na ushindi huo wa mabao 5-0.

Mabao mawili ya Tembo Warriors yalifungwa na  Alfan Kiyanga dakika ya  pili na 15 na mengine ni Ramadhan Chomole dakika ya  18 na Frank Ngailo  dakika ya  36 na  44.

 

Katika mechi zote za mashindano Tembo Warriors imepoteza mechi moja tu dhidi ya Uganda ambayo walifungwa bao1-0.  Tembo waliifunga Morocco 2-1 na Sierra Leone 1-0.

Mchezo huo wa jana ulishuhudiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassani Abassi na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu Duniani (WAFF), Mateus Widlak.

Akizungumza  baada ya mchezo huo, Bashungwa alisema Tembo Warriors imetoa funzo kwa timu nyingine kuhakikisha zinafanya vizuri na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwasaidia  ili iendelee  kufanya vizuri  maandalizi ya Kombe  la Dunia.

Pia aliwaahidi Sh 200,000 kwa kila mchezaji baada kukata tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

 

"Rais Samia Suluhu Hassan anawapongeza kwa kufuzu na nyie mmetoa funzo kwa timu nyingine kuhakikisha zinafanya vizuri kama ninyi, serikali itaendelea kuwa pamoja na ninyi katika maandalizi ya kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Uturuki," alisema Bashungwa.

Mashindano hayo ambayo yanashirikisha mataifa 14 yatatoa timu nne zitakazowakilisha Afrika katika Kombe la Dunia kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 5.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/af0ae7f7c9e25339ccf18256d1ece9a9.jpeg

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi