loader
GGML yachangia milioni 84/- mapambano dhidi ya Ukimwi

GGML yachangia milioni 84/- mapambano dhidi ya Ukimwi

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imechangia zaidi ya Sh milioni 84 kusaidia mipango ya serikali katika mapambano na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya juzi.

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) na GGML kupitia kampeni ya Kilimanjaro Challenge zimekuwa zikishirikiana kwa namna mbalimbali ikiwamo kuongeza uelewa kuhusu janga la VVU na Ukimwi ili siku moja Tanzania itangazwe kuwa imetokomeza kabisa janga hilo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho hayo jijini Mbeya, Makamu wa Rais wa GGML anayeshughulikia miradi endelevu, Simon Shayo alisema kaulimbiu ya mwaka huu isemayo ‘Zingatia usawa, tokomeza Ukimwi, tokomeza magonjwa ya mlipuko’ ni muhimu kwa jamii ya Geita na Tanzania kwa ujumla. Alisema GGML Kili Challenge ni mradi mahususi kutoka katika sekta binafsi ambao umeisaidia serikali kwa zaidi ya miaka 20 katika mapambano dhidi ya VVU.

“Kupitia mpango huu, wachangiaji wenzetu wameendelea kuwa mstari wa mbele kudhibiti janga la VVU kwa kuhakikisha utoaji huduma za kimatibabu unazingatia utu na haki za wale wote wanaoweka imani yao kwetu hususani wale walio hatarini zaidi,” alisema. Alisema GGML pia iliandaa kampeni ya upimaji wa VVU kwa hiari kwa wiki mbili ikilenga kufikia asilimia 80 ya wafanyakazi wake 5,000 walioajiriwa moja kwa moja na wakandarasi.

Shayo alisema maendeleo chanya ya kijamii na kiuchumi ya mkoa na nchi ni matokeo ya jamii yenye afya. Alisema kuanzia Desemba Mosi hadi 14, mwaka huu, GGML imealika washauri nasaha 15 waliopata mafunzo ya Ukimwi kutoka serikalini na hospitali binafsi ili kufanya upimaji wa VVU kwa hiari katika eneo lote la mgodi huo. GGML Kilimanjaro Challenge dhidi ya VVU na Ukimwi ilizinduliwa zaidi ya miaka 20 iliyopita kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii juu ya janga hilo na kutoa msaada wa kifedha katika mapambano hayo.

Kilimanjaro Challenge imebadilika na kushirikisha kampuni za ndani na nje ya nchi na watu binafsi kutoka duniani kote hali iliyosaidia kuchangisha zaidi ya Sh bilioni 1.3 tangu 2018 kwa ajili ya miradi ya kinga, matunzo na matibabu ya VVU nchini kote.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ac7d06343ff67b1c18fd9ccfb70555bc.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi