loader
Abiria 633,000 kutumia mwendokasi Mbagala kila siku

Abiria 633,000 kutumia mwendokasi Mbagala kila siku

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema abiria 633,000 wanatarajiwa kutumia usafiri wa mabasi ya mwendo kasi kwa siku kupitia mradi wa pili wa BRT unaohusisha njia 30 kutoka Mbagala hadi Gerezani.

Tathimini ya haraka iliyofanywa na mamlaka imeonesha watu watakao tumia njia hizi kwenda na kurudi inakadiriwa kufika 673,800 kwa siku. “Kitendo ulichofanya leo cha kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huu kinaenda kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi wa Dar es Salaam hususani ukanda wa Mbagala na Gerezeni,” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy Mwalimu amemwambia Rais Samia kuwa ofisi yake inakusudia kuweka magari 755 ya mwendokasi katika awamu ya pili ya mradi huo ili kuongeza ubora wa huduma za usafiri, ufanisi na kwa haraka zaidi.

Waziri Ummy amesema katika idadi hiyo mabasi makubwa yanatarajiwa kuwa 250 na yale yenye urefu wa mita 12 yatakuwa 500.

Amesema kutokana na idadi hiyo kubwa, serikali imeona haja ya kuongeza idada ya karakana kutoka moja iliyojengwa eneo la Mbagala rangi tatu hadi mbili ambapo nyingine itajengwa eno la Kurasini.

“Tunao uwezo na uzoefu wa kutoa huduma za usafiri kupitia mradi wa BRT Gerezani- Kimara, Gerezani-Feri. 

Huduma ya awamu ya pili kwa wakazi wa Dar es Salaam kutoka Mbagala- Gerezani zitakuwa huduma bora, za ufanisi na haraka zaidi,” amesema na kuongeza kuwa idadi ya njia 11 zitakuwa ni za barabara kuu na njia zingine 19 zitakuwa za mrisho.

kwa upande mwingine, serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kuanza utekelezaji wa mpango wa kuunganisha kituo kikuu cha gari moshi cha kisasa na barabara za mwendokasi (BRT) ili kufungamanisha huduma za usafiri kwa abiria.

“Katika kituo kikuu cha treni ya mwendo kasi (SGR) tumeweka kituo cha mabasi ya mwendokasi ili kufungamanisha usafiri wa SGR na mwendokasi. tumeanza maandalizi ya kukamisha jambo hili,” amesema Waziri Ummy wakati wa Haflya ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka, Awamu ya Pili, Mbagala Rangi Tatu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/89a55bb304979b19417f71c65e7b7950.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi