loader
Simba rekodi nyingine Caf

Simba rekodi nyingine Caf

MIAMBA ya soka nchini, Simba imeweka rekodi nyingine katika Michuano ya Afrika baada ya jana kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Simba imetinga hatua hiyo baada ya `kubebwa’ na ushindi wa nyumbani wa mabao 3-0 baada ya jana ugenini kufungwa 2-1 na Red Arrows ya Zambia na kushinda kwa jumla ya mabao 4-2.

licha ya kufungwa 2-1 na imetinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuiondoa Red Arrows ya Zambia kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2. Simba iliaanza michuano hiyo kwa kuishinda timu hiyo nyumbani kwa mabao 3-0 wiki iliyopita na katika mechi ya marudiano iliyochezwa jana nchini Zambia ikalala kwa bao 2-1, hivyo kuingia hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 4-2.

Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuweka rekodi hiyo katika vitabu vya kumbukumbu. Simba imeendelea kuwa mwiba kwa timu za Zambia katika mashindano ya CAF na Red Arrows inakuwa timu ya tatu kuondolewa katika mashindano tofauti baada ya Mufulila Wanderers kuondoshwa kwa mabao 5-4 mwaka 1979 na Nkana kwa mabao 4-3 mwaka 2018 ambazo ziliondoshwa katika Ligi ya Mabingwa.

Red Arrows jana walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 44 mfungaji akiwa Ricky Banda, ambaye aliachia shuti kali baada ya kupokea mpira wa kurushwa wa beki Mubili Nickson na hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Red Arrows wakiliandama lango la Simba na jitihada zao zilizaa matunda katika dakika ya 47 baada ya Saddam Phiri kufunga kwa kichwa akimalizia krosi ya Ricky Banda.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0b574dbd69372d391fdde1943c7d175e.jpeg

ZIMEBAKI pointi mbili, Mbeya City iwafikie Simba SC ...

foto
Mwandishi: Na Martin Mazugwa

Post your comments