loader
TBA yajiridhisha kasi ya ujenzi nyumba 3,500

TBA yajiridhisha kasi ya ujenzi nyumba 3,500

KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Miliki ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Said Mndeme ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa nyumba 3,500 na nyumba 20 za viongozi zinazojengwa jijini Dodoma na wakala huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa baada ya kukagua ujenzi wa nyumba hizo, Mndeme alionesha kuridhishwa na kazi ya wakala na jinsi walivyojipanga kutekeleza miradi hiyo kwa kuwa na vifaa vya kutosha na vya uhakika.

“Tumeridhika kwa jinsi ambavyo wamejipanga. Kuna saruji na nondo za kutosha, hivyo hatuna sababu ya kuwa na vikwazo vyovyote. Binafsi nimeridhika na nimefurahi katika kuhakikisha tunapunguza gharama na kutekeleza miradi kwa ubora.”

“Tumeona mna kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha tofali 6,000 kwa wakati mmoja, jambo ambapo litatusaidia kuwa na tofali zenye ubora na pia mna mashine ya kisasa ya kuchanganya zege,” alisema.

Kwa upande wa mradi wa Nzuguni wa nyumba 3,500, Mndeme alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 150 imeanza kwa ujenzi wa nyumba 86. “Nyumba hizi 3,500 zitakuwa za kisasa. Kutakuwa na ujenzi maghorofa 100 na nyumba kubwa 200 na nyumba za ukubwa wa kati 1,400, maghorofa yatakuwa nyumba tofauti tofauti 800 na za ukubwa wa chini ni nyumba 1000.”

Mndeme alisema katika eneo hilo kutakuwa na huduma za kijamii ambapo kutajengwa shule za awali tano, nyumba za ibada; misikiti na makanisa, soko na kituo cha biashara.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/04f3ec88c755e124c017fca06bb7a19b.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi