loader
Sensa mwakani inakwenda kidijiti

Sensa mwakani inakwenda kidijiti

S ENSA ya sita itakayofanyika Agosti mwakani, itakuwa ya kiditi. Akizungumza katika maeneo tofauti wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakati akihamasisha wananchi kushiriki katika sensa ya watu na makazi mwakani, Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda alisema sense ya mwaka huu si ya makaratasi.

“Sensa zilizopita zilitumia makaratasi ya dodoso katika kukusanya taarifa na takwimu mbalimbali kutoka kwa wananchi, lakini sensa ya mwakani, itakuwa ya kidijiti kwa sababu itatumia vishikwambi (tablets),” alisema.

Spika huyo mstaafu wa Bunge alisema, makarani ambao wameelimishwa na kulishwa viapo vya uaminifu na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) watakuwa na vishikwambi kwa ajili ya kukusanya takwimu mbalimbali na muhimu kwenye kaya katika ngazi za vitongoji na mitaa.

Takwimu zitakazokusanywa na makarani hao ni za watu wote ambao watakuwa wamelala ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Tanzania usiku wa kuamkia siku ya sensa Agosti mwakani katika tarehe ambayo Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa ametangaza hapo baadaye.

Makinda alisema, makarani hao wakikusanya takwimu watatuma moja kwa moja kwenye kompyuta maalumu (sever) katika Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) kitakachokuwa kituo maalumu cha kupokea na kuhifadhi taarifa kutoka kwenye kaya mbalimbali za vitongoji na mitaa.

Makinda alisema, kutokana na kuwa sensa ya kidijiti, ukusanyaji wa takwimu utafanyika kwa haraka, kwa gharama nafuu na hata haitachukua muda mrefu kuzichambua taarifa hizo na kuanza kutumika. Alisema tofauti na sensa zilizotangulia ambazo takwimu zilikusanywa kutika ngazi ya wilaya, sensa ya mwakani takwimu zake zitakusanywa katika ngazi ya vitongoji na mitaa na hivyo takwimu nyingi na kwa uhakika zaidi zitapatikana.

Kwa sasa utengaji wa maeneo unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ili kujua ni maeneo kiasi gani kama vitongoji na mitaa itatumika katika kukusanya takwimu hizo. Sensa ya mwisho ilifanyika 2012 na nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988 na 2002.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6ba4e7de21d4be42c8d84f17647a29db.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi