loader
Samia apokea kilio barabara za vumbi kigamboni

Samia apokea kilio barabara za vumbi kigamboni

RAIS Samia Suluhu Hassan amepokea kilio cha wananchi wa Kigamboni kuhusu changamoto ya barabara na kumtaka Mbunge wa Jimbo la Kigamboni kusaidia kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23.

“Tunachangamoto ya barabara,” Dk Faustine Ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni alimwambia Rais Samia wakati aliposimama Kibada kuzungumza na Wananchi. 

“Kigamboni tuko nyuma sana katika miundombinu ya barabara. Katika barabara za Tarura, asilimia 37 tu ya barabara zimepigwa lami. Na katika asilimia 100 ya barabara za vumbi mkoa wa Dar es Salaam, asilimia 50 zipo wilaya ya Kigamboni.  

Sambamba la hilo, tuna barabara za ndani, na kwetu asilimia 70 ya mji umepiwa. Ila katika miundombinu ya Tarura tuna zaidi ya kilometa 1000 lakini zilizopigwa lami ni kilometa 5 sawa na asilimia 0.5.

Kipaumbele changu cha kwanza ni barabara na cha pili ni barabara na tatu ni barabara,” alisema Ndugulile.

Rais Samia amesema changamoto ya barabara za lami ipo maeneo mengi na kwamba ni hivi karibuni, maeneo mengi ya Mkoa ya Dar es Salaam yameanza kuwekewa lami. 

“Miaka mitano sita iliyopita ndio imeanza kufunguka kwa lami. Kigamboni kwa kuwa ni eneo jipya hatushangai kuona hakuna sehemu kubwa ya lami. Lengo letu mkoa mzima wa Dar es Salaam uwe na lami kwa sababu Dar es Salaam ndio lango la biashara,” amesema na kuongeza kuwa tunafungua Kigamboni kwa viwanda na hivyo ni lazima kuwe na barabara za lami.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/cefa2409fe55e9ddd85df0b1b5843e26.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi