loader
Waamuzi ligi kuu wamduaza Waziri Bashungwa

Waamuzi ligi kuu wamduaza Waziri Bashungwa

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwachukulia hatua waamuzi wanaofanya maamuzi ya hovyo katika michezo mbalimbali.

Waziri Bashungwa amezungumza hayo mbele ya waandishi wa habari katika kilele cha mashindano ya kitaifa ya Michezo na Sanaa ya vyuo vya ualimu UMISAVUTA yaliyofanyika Mtwara kuanzia Novemba 29, 2021.

Amesema licha ya Ligi Kuu kuendelea vizuri lakini kumekuwa na waamuzi wanaofanya mambo ya hovyo ambayo siyo tu yanashusha hadhi yao lakini yanavunja imani, amani na mioyoo ya wachezaji na mashabiki.

 “ We fikilia kuna klabu unakuta inachangishana Sh elfu 10, au elfu tano ili hiyo klabu ikacheze sehemu fulani, inatoka Mkoa A inaenda Mkoa B alfu mwamuzi anafanya mambo ya uonevu uwanjani, hilo jambo linamuumiza,”amesema Bashungwa.
 
Akizungumzia mashindano ya UMISAVUTA, Waziri Bashungwa amesema Wizara yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha mahitaji ya walimu wa michezo shuleni yanaendana na uzalishaji wa walimu hao kwenye vyuo wa ualimu.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo amesema dhamira ya kurejeshwa kwa mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesitishwa kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, ni kuwatengeneza walimu wanafunzi, kuwa imara katika michezo wenye ujuzi na uwezo wa kushiriki na kuendesha michezo katika shule watakazopangiwa pindi wanapo hitimu masomo yao.


Mwenyekiti wa mashindano hayo kwa mwaka 2021, Doroth Mhaiki amesema matarajio yao ni kuona vyuo vya ualimu Tanzania vikishiriki katika mashindano mbalimbali ya Afrika Mashariki.


Mashindano hayo ya UMISAVUTA yameusisha Michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mpira, riadha, fani za ndani na mashindano ya ubunifu wa vifaa vya kufundishia ambapo kanda ya Mashariki imeibuka bingwa katika mchezo wa soka huku Kanda ya Ziwa ikiibuka mshindi wa jumla kwa kubeba vikombe vingi zaidi katika mashindano hayo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8f139f80071faa1e9219f2747721fd11.jpg

ZIMEBAKI pointi mbili, Mbeya City iwafikie Simba SC ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments