loader
Songwe wajitosheleza  kwa chakula

Songwe wajitosheleza kwa chakula

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema wanajivunia kujitosheleza kwa chakula na kushika nafasi ya tano kitaifa kwa pato la wananchi wake hivyo kuboresha uchumi wao.

Mgumba alisema hayo alipokuwa akizungumzia mafanikio ya mkoa huo ndani ya miaka 60 ya uhuru.

"Kama mnavyofahamu kabla ya uhuru na mwanzoni mwa miaka ya  uhuru nchi hii ukiwamo Mkoa wa Songwe kwa sasa  tulikuwa na  changamoto kubwa sana ya utoshelevu wa chakula, hatukuwa na uwezo wa kujilisha mwaka mzima pamoja na jitihada kubwa za wananchi hususani wakulima waliokuwa wanalima kwa ajili ya chakula chao na ziada kulisha taifa,” alisema.

Mgumba alisema miaka 60 ya uhuru kwa mujibu wa takwimu nchi inajitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada zaidi ya asilimia124, huku Mkoa wa Songwe ukiwa na mchango mkubwa katika mafanikio hayo kwa taifa.

"Mkoa wa Songwe ni wa tatu kwa kilimo cha mahindi nchini ambayo ndio chakula kikuu kwa jamii kubwa ya Watanzania, pia mkoa wetu ndio namba moja nchini kwa matumizi ya mbolea ambayo imeweza kuongeza tija  na uzalishaji mkubwa na kipato cha mwananchi mmoja mmoja kuongezeka kushinda mikoa mingine nchini," anasema Mgumba.

Mshauri wa uchumi na uzalishaji Mkoa wa Songwe, Vasco Kulanga alisema kitakwimu mkoa huo unashika nafasi ya tano kitaifa kwa pato la wananchi wake, hivyo kuwa miongoni mwa mikoa ambayo wananchi wake wana kipato cha juu.

Alisema mkoa huo umeweka kipaumbele mazao ya chakula na biashara ili wananchi kwenye kila wilaya angalau wawe na zao moja ama zaidi ya kuingizia kipato.

Alisema serikali imeendelea kujenga miundombinu na kuwa kichocheo cha ukuaji wa sekta mbalimbali ikiwamo  usafirishaji na uchukuzi, safari za ndege katika Uwanja wa Songwe na kuwapo umeme wa uhakika na kufunguliwa mabenki.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/daa56a9ed2e6519b2067979487a053bc.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Baraka Messa, Songwe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi