loader
TCRA yaeleza faida Sheria Makosa ya Mtandao, Miamala Kielekroniki

TCRA yaeleza faida Sheria Makosa ya Mtandao, Miamala Kielekroniki

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kupitishwa kwa Sheria ya Makosa Mtandaoni 2015, Sheria ya Miamala ya Kielektroniki na Sheria ya Usalama wa Mtandao kumechangia kuinua nafasi ya Tanzania kimataifa katika masuala ya usalama mtandaoni.

Ofisa Mwandamizi wa TCRA, Semu Mwakiyanjala alisema jijini Mwanza jana kuwa, mwaka jana Tanzania ilikuwa ni nchi ya pili kwa usalama mitandaoni ikiwa imepanda kutoka nafasi ya 12 mwaka 2017.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika na maendeleo katika sekta ya mawasiliano nchini.

Alisema sehemu ya masafa yaliyopatikana baada ya uhamaji huo yaliuzwa kwa mnada kwa kampuni mbili zilizoshinda na zilizotakiwa kufikisha huduma za mawasiliano ya kasi kwa angalau asilimia 60 ya Watanzania hadi mwishoni mwa mwaka huu na asilimia 90 ifikapo mwaka 2024, lengo kubwa likiwa kupanua upatikanaji wa masafa na matumizi ya intaneti.

Alisema shughuli kuu za kiusimamizi na uendelezaji wa sekta zilizofanyika miaka ya hivi karibuni ni pamoja na uboreshaji wa laini za simu kibiometria, lengo likiwa ni kuwa na kanzidata imara ya kuaminika kwa watumiaji wa laini hizo na vifaa vya mawasiliano vinavyotumia laini ili kuendeleza sekta hiyo, kulinda watumiaji na kudhibiti matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano.

Mwakyanjala alisema mfumo mpya wa leseni usioegemea teknolojia ulioanzishwa na serikali mwaka 2005 umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa kasi ya maendeleo ya sekta ya mawasiliano nchini.

Alisema tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 1961, kuna wenye leseni za kuweka miundombinu 23, leseni za simu za mikononi na mezani ambapo hadi sasa kuna jumla ya kampuni saba zilizosajiliwa na zinatoa huduma.

“Kwa sasa tuna leseni za huduma tumizi za mawasiliano 79, redio 205 na vituo vya televisheni 51 vinavyorusha matangazo bila kulipia,” alisema.Alisema maboresho mengine yaliyofanyika katika sekta hiyo ni kupitishwa kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca) iliyopitishwa mwaka 2010 ili kuimarisha misingi ya usimamizi wa masuala mengi yakiwamo ya usajili wa matumizi ya laini za simu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7a7c977a2d2b5b06f2e190652095e38a.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi