loader
CHRAGG yataka haki za binadamu uwekezaji, biashara

CHRAGG yataka haki za binadamu uwekezaji, biashara

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) imesema haki za binadamu katika uwekezaji na biashara bado ni changamoto, hivyo kutaka mkakati wa pamoja baina ya wadau ili kuweka mikakati ya kulinda haki hizo.

Imesema tathmini zilizofanywa zimebaini kuwapo kwa ukiukwaji wa haki hizo katika maeneo ya uwekezaji kama hotelini, katika migodi, viwanda na kwingineko licha ya kuwapo sheria zinazotaka kuhakikisha haki hizo zinatekelezwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alisema hayo wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya tume hiyo, wafanyabiashara, asasi za kiraia na wadau mbalimbali.

Alisema tume hiyo imekuwa ikifanyakazi kukuza haki za binadamu katika biashara na mwaka jana ilifanya tathmini na ukaguzi kuhusu haki hizo katika wilaya za Namtumbo Mkoa wa Ruvuma, Kilombero Mkoa wa Morogoro  na Kahama Mkoa wa Shinyanga.

“Katika tathmini na uchunguzi tuliofanya, serikali na wadau wa biashara walikumbushwa wajibu wao wa kulinda na kuheshimu haki za binadamu linapokuja suala la biashara,” alisema.

Alisema kuna ukiukwaji wa haki za biashara katika migodi ambayo inatakiwa kuwa na vifaa maalumu kulinda afya, mikataba ya ajira ili kuzuia  kufukuzwa wafanyakazi bila kufuata utaratibu, pamoja na masuala mengine ikiwamo kwa wenye viwanda kutiririsha kemikali kutoka viwandani hivyo kuathiri haki za wananchi walio karibu.

Ofisa Mipango wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Hassan Ameir Vuai alisema kumekuwa na changamoto za ukiukwaji wa haki za biashara kwa wawekezaji kutokana na kutofuata sheria.

“Kati ya vitendo vya ukosefu wa haki za binadamu kwa wawekezaji ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, kutokuwa na mikataba ya kazi pamoja na kufukuza kazi bila kufuata sheria za kazi, lakini sasa tunachofanya ni kutoa elimu kwa wawekezaji ili kulinda haki za binadamu  kuleta tija na ustawi katika biashara,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b8f541150c0efb465f83128bca5726b1.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi