loader
Maandalizi tuzo za filamu yapamba moto

Maandalizi tuzo za filamu yapamba moto

BODI ya filamu Tanzania imesema maandalizi ya tuzo za filamu zinazotarajiwa kufanyika Disemba 18 mkoani mbeya yanaendelea vizuri huku msafara kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya ukitarajiwa kuwasili Disemba 15.

Aidha katika hatua nyingine Bodi hiyo imemtangaza msanii wa filamu Yvonne Cherryl (Monalisa) kuwa balozi wake ambapo pamoja na mambo mengine majukumu yake yatakuwa kutangaza mambo mbalimbali ya bodi hiyo.

Akizungumzia maandalizi hayo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dk Kiagho Kilonzo amesema kuelekea katika tuzo hizo ambazo mwaka huu zinafanyika chini ya usimamizi wa Serikali kila kitu kinakwenda sawa huku kamati mbili za maandalizi zikitarajiwa kukutana jana.

"Kimsingi kamati hizi moja kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na nyingine ya hapa Dar es Salaam zinakutana leo kwa ajili ya kukamilisha mipango ya mwisho ya maandalizi ya tuzo hizo, nisisitize kwa kusema kuwa hadi sasa kila kinakwenda sawa" alisema Dk Kilonzo

Alisema matarajio msafara mzima utakaohusisha wasanii na watu mbalimbali unatarajia kuondoka Dar es Salaam Desemba 14 kwa kutumia usafiri wa treni ya Tazara na kisha kufika Mbeya siku inayofuata.

Alisema Desemba 16 na 17 wasanii nao na msafara mzima wanatarajiwa kuwa na ziara katika maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyopo katika mkoa huo ikifuatiwa na chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Aidha Dk Kilonzo akimtangaza Monalisa kuwa Balozi wa Bodi hiyo, alisema lengo ni kuona mambo mbalimbali ya bodi hiyo yanatangazwa vizuri kupitia kwa balozi wake huyo aliyepo katika tasnia ya filamu kwa zaidi ya miaka 23 hadi sasa.

Amesema kwa kipindi kirefu taasisi ilikosa balozi ambaye ndiye atakuwa na kujumu la kuiongelea taasisi kupitia mitandao ya kijamii, matamasha, semina, kuongea na vyombo vya habari na masuala mengine na kwamba kupatikana kwa Monalisa ni furaha kwa taaisi hiyo.

Kwa upande wake Monalisa alisema hatua ya yeye kuteuliwa kuwa balozi wa bodi hiyo kumemfarijisha huku akiahidi kitumia nafasi aliyonayo kuitangaza bodi hiyo kikamilifu.

Amesema kuna wasanii wengi na wenye sifa mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kupewa nafasi hiyo lakini kitendo cha yeye kupewa nafasi hiyo kimemfanya ajione kuwa mwenye heshima kubwa.a

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ce59d3dbcef0c557a71f82f9819151bf.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi