loader
Wadau wajadili changamoto za watoto walemavu.

Wadau wajadili changamoto za watoto walemavu.

.....jamii yatakiwa kutowaficha.

 

JAMII imetakiwa kutoficha watoto walemavu na badala imetakiwa kuwatambua na kuacha kuwaficha nyumbani.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la Light For the World Tanzania linaloshugulika na masula ya watoto walemavu Joseph Banzi katika kongamano la kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili watoto walemavu ili wasiachwe nyuma katika dunia ya teknolojia na utandawazi                                            

Banzi amesema watoto walemavu wanakumbana na changamoto mbali mbali za elimu jumuhishi na wengine wanashindwa kuendelea na masomo yao.

Amesema ukosefu wa miundombinu rafiki yakujifunzia katika shule jumuishi nchini ni changamoto hivyo uathiri maendeleo ya watu wenye ulemavu.

Amesema kuwa mfumo wa elimu maalaumu unachangamoto nyingi ndiyo maana jamii imetakiwa kufahamu umuhimu wa mfumo wa elimu jumuishi pamoja na kwamba miundombinu ni changamoto kwao

Banzi amesema kuwa mfumo wa elimu maalumu unaweza kuchangia baadhi ya watoto kukosa haki za msingi kutokana na umri lakini pia kupoteza asili na tamaduni zao kwa kusoma mbali na nyumbani kutokana na wazazi wengi kuwapeleka watoto shule maalumu na kuwatelekeza watoto huko.

Amesema shirika lao linashugulika na watoto wenye uoni hafifu ambapo asilimia 70 wanawasaidia katika masomo yao na ufaulu kwenda sekondari.

“Kwa sasa tuna watoto 311 katika mkoa wa Morogoro na Dodoma, sera ya serikali inasaidia kutoa fursa kwa walemavu kwa sasa, inatia mkazo haachwi mtu nyuma, inatoa mwongozo kwa elimu jumuishi imesaidia watoto walemavu kusoma na kufikia lengo namba 4 ambalo kila mtoto apate elimu.”amesema Banzi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), Hernest Kimaya amesema bado kuna changamoto kwa watu wenye ulemavu na kwamba kongamano hilo la majadiliano litasaidia kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili walemavu  ili wasome bila shida na kufikia malengo yao.

Ametaja baadhi ya changamoto hizo ni ukosefu wa walimu na  vifaa vya kufundishia

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d0377c6a74c5cf69a1c57f807434b014.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi