loader
China yaisifu Tanzania ushirikiano na Afrika

China yaisifu Tanzania ushirikiano na Afrika

SERIKALI ya China imesifu ushiriki wa Tanzania kwenye Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Focas) na nchi hizo mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja za miundombinu, afya, biashara, uwekezaji na mambo mengine mbalimbali.

Pongezi hizo zilitolewa na Balozi wa China nchini, Chen Mingjian kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao jana.

Alisema Tanzania ni mwanachama muhimu wa Focas na katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa jukwaa hilo uliofanyika Dakar, nchini Senegal mwishoni mwa mwezi uliopita, ilitoa mchango muhimu katika kufanikisha mkutano huo chini ya ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula.

Alisema wakati wa mkutano huo, Balozi Mulamula alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ambapo walikubaliana nchi hizo mbili kuimarisha ushirikiano wao katika miundombinu, afya, biashara, uwekezaji na nyanja nyingine.

Alisema mawiziri hao pia walikubaliana kufuata mwongozo wa maafikiano kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa China, Xi Jinping wakati wa mazungumzo yao ya simu Juni, mwaka huu.

Katika mazungumzo yao, Rais

Samia na Rais Xi walikubaliana Tanzania na China kukuza ushirikiano katika uchumi, utamaduni na ushirikiano wa kimataifa, ambapo China iliahidi kufungua zaidi soko lake kwa bidhaa za Tanzania na kuongeza uwekezaji hususan katika sekta ya viwanda.

“China na nchi 53 za Afrika pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) walijadili mambo muhimu sana kwa ushirikiano kati ya China na Afrika na kutafuta njia bora za kukuza maendeleo ya pamoja ya China na Afrika. Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo na kutoa mchango muhimu katika kuufanikisha mkutano huo,” alisema Balozi Mingjian.

Pia alisema Rais Xi alihudhuria hafla ya ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya mtandao ambapo alisisitiza moyo wa urafiki na ushirikiano wa dhati kati ya China na Afrika, manufaa ya pamoja ya maendeleo kwa pande zote, usawa, haki, uwazi na ushirikishwaji.

Kwa mujibu wa Balozi Mingjian, Rais Xi alitangaza programu tisa zitakazotekelezwa kwa pamoja kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo.

Alizitaja programu hizo ni afya, kupunguza umaskini, maendeleo ya kilimo, kukuza biashara, kukuza uwekezaji, uvumbuzi wa kidijitali, maendeleo ya kijani, kujenga uwezo, utamaduni, amani na usalama na ushirikiano wa mtu na mtu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7089538c4965f6bfb1de04f9ea32ca86.jpeg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: China Na Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi