loader
Samia aipa saluti Tembo Warriors

Samia aipa saluti Tembo Warriors

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kufuzu kombe la dunia kwa timu ya soka ya taifa ya watu wenye ulemavu ni heshima kubwa kwa taifa.

Rais Samia alitoa kauli hiyo Ikulu Dar es Salaam jana alipoipongeza timu ya soka la watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ kwa kufuzu Kombe la Dunia Uturuki, mwakani.

Tembo ilikata tiketi hiyo baada ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Afrika iliyofanyika nchini wiki iliyopita.

Rais Samia aliialika timu hiyo Ikulu kutoa pongezi zake kwa kuwa timu hiyo.

Alisema, alikuwa anafuatilia mashindano hayo kwa karibu na kumuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jicho lake kwa karibu ili wanamichezo hao kutoka Mataifa 12 ya Afrika wasipate shida nchini.

“Naambiwa timu hii imeanzishwa mwaka 2018 lakini ninyi mmefuzu Kombe la Dunia, kufuzu Kombe la Dunia ni kombe la dunia, haijalishi unacheza mchezo gani hata kama ni bao,” alisema.

“Kuna timu zimeanzishwa kabla ninyi wengine hapa hamjazaliwa na hawajaenda Kombe la Dunia hivyo hongereni sana na tutaendelea kuwatunza ili mkashiriki vizuri kwani mmetoa somo kwa Watanzania kuwa mnaweza na mmeandika historia,” alisema Rais Samia.

Rais alisema Mungu akikupa ulemavu hakunyimi mwendo hivyo maumbile watu wote wako sawa isipokuwa maumbo ndio tofauti na ulemavu haukuzuii kufanya vizuri.

Alisema kufuzu kwa Tembo Warriors, Kombe la Dunia ni moja ya utekelezaji wa michezo katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuagiza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha inawalea vizuri ili wakienda Kombe la Dunia wakafanye vizuri.

Aliwaasa wachezaji hao kukumbuka wanapocheza nyumbani au ugenini kazi yao ni kupeperusha bendera ya Taifa na kuwaahidi kuwatafutia mlezi atakayekuwa nao kila wakati.

Baada ya pongezi hizo Rais Samia aliwapa wachezaji na viongozi nauli na kuwatakia mafanikio zaidi.

Katika mashindano haya ambayo yalishirikisha nchi 14, Tembo Warriors ilishika nafasi ya nne na kutoa mchezaji bora, Frank Ngailo pia kufuzu Kombe la Dunia.

Bingwa katika mashindano hayo ni timu ya Taifa ya Ghana ambao waliifunga Liberia kwa mabao 3-2 lakini haitashiriki Kombe la Dunia kwa sababu siyo mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu duniani (WAFF) badala yake nafasi yake ilichukuliwa na mshindi wa tano timu ya Taifa ya Morocco akiungana na Liberia, Tanzania na Angola kushiriki Kombe la Dunia.

Timu 14 zilizoshiriki michuano hiyo ziligawanywa kwenye makundi manne.

Kundi A liilikuwa Tanzania, Sierra Leone, Uganda na Morocco, Kundi B lilikuwa na Angola, Kenya, Rwanda na Zanzibar, Kundi C lilikuwa na timu za Liberia, Cameroon na Gambia na Kundi D ni Nigeria, Ghana na Misri.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8420e5072595b1d27322476ef26dfcb1.png

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi