loader
Dk Gwajima aishukuru Serikali ya Marekani

Dk Gwajima aishukuru Serikali ya Marekani

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Sekta ya Afya hususani afua za kujikinga na virusi vya Ukimwi na kununua dawa za kufubaza virusi hivyo.

Dk Gwajima ametoa shukran hizo leo Disemba 8, 2021 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini, Dk Donald Wright akiwa ameambatana na ujumbe wake kwa lengo kujadili jinsi Wizara ya Afya itakavyoweza kuendelea kuimarisha ushirikiano katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.

 

Dk Gwajima amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania inaendelea vizuri katika suala la kupambana na UVIKO-19 ambapo hadi hivi sasa chanjo zaidi ya 4,000,000 zimesambazwa kwenye zaidi ya vituo 6,000.

Amesema kuwa takribani wananchi 1,159,462 wameshapata chanjo kamili sawa na asilimia 65 ya chanjo zilizopokelewa.

Aidha, Dk Gwajima amesema maabara za jamii za upimaji wa virusi hivyo zimeongezeka na Serikali iko mbioni kuanza huduma za upimaji katika Hospitali za Rufaa za  Mikoa.

Akizungumzia anuai mpya ya UVIKO ya Omicron, Dk Gwajima amesema Serikali ya Tanzania imeimarisha mfumo wa ufuatiliaji kwa wahisiwa wa ugonjwa huo kwa kuweka wataalamu wa afya kwenye maeneo muhimu ikiwemo Viwanja vya Ndege,Vituo vya Magari na Bandari zote hapa nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani hapa nchini Dk Donald Wright amesema kuwa Serikali ya Marekani inatumia Dola milioni 400 kwa mwaka kufadhili miradi ya afya ambapo imesaidia watu milioni 1.5 kuwapatia dawa za kufubaza virusi vya  ukimwi na kwamba Marekani ina mpango wa kutoa dawa ya kukinga Virusi vya Ukimwi.

Aidha Dk Wright ameihakikishia Tanzania kuendeleza ushirikiano na kwamba ipo wazi kupokea vipaumbele vya nchi katika kuhakikisha wanakabiliana na magonjwa hatarishi kwa jamii na kwamba ameishauri Serikali ya Tanzania kuhakikisha inaendendea kuweka huduma za Chanjo ya UVIKO 19 kwenye vituo vyote vya kutoa huduma za Afya kwa lengo la kuwafikishia watu wengi zaidi ili kuokoa maisha ya watu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/480ba4fe9df0b8cb2f15be3a339b3071.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi