loader
Tanapa kuhamisha wanyama kwenda Hifadhi Tarangire

Tanapa kuhamisha wanyama kwenda Hifadhi Tarangire

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeeleza kuwa katika hatua za mwisho za kuwahamisha wanyama pori aina ya Nyumbu na Pundamilia kutoka Pori Tengefu na kuwapeleka Hifadhi ya Tarangire kutokana na ufinyu wa eneo la malisho ndani ya Hifadhi ya Ziwa Manyara.

Katika taarifa yao, Tanapa wameeleza kuwa changamoto hiyo imetokana na mvua zilizonyesha mwaka 2019-2020 na kusababisha maji kufurika eneo la ziwa na kusababisha wanyama kubaki nje ya hifadhi.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Nyumbu 370 na Pundamilia 151 wapo kwenye Pori Tengefu Mto wa Mbu, ambako pia ni jirani na makazi ya watu katika maeneo ya Migugani, Loswira na Ngogoro ambayo yana uhaba wa malisho kutokana na ukame.

Aidha, mwishoni mwa mwezi Novemba viliibuka vifo vya wanyama kadhaa, katika eneo la Migungani vilivyosababishwa na ukosefu wa eneo la malisho na ukame.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/26d231d20865fa31639b394449441a61.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi