loader
'The Rock' ang'ara Tuzo za Chaguo la Watu

'The Rock' ang'ara Tuzo za Chaguo la Watu

MWANAMIELEKA na Muigizaji Maarufu Dwayne Johnson ama “The Rock” ndiye Chaguo la watu kulingana na Tuzo ya Chaguo la Watu 2021 (The People’s Choice Award).

The Rock alitwaa kikombe cha Muigizaji bora wa kiume na nyota wa Filamu ya Vichekesho kwa mwaka 2021.

Tuzo hizo za kila mwaka ambazo hutokana na kura za mashabiki zilijumuisha vipengele 40 vya burudani vikihusisha filamu, televisheni, muziki na utamaduni. 

Christina Aguilera, alipokea Tuzo ya Heshima ya Muziki ‘inaugural Music Icon Award,’ Mwanamitindo na muigizaji, Halle Berry, alipata  Tuzo ya Watu ‘People's Icon Award’, na Kim Kardashian, alipata Tuzo ya Mitindo.

Katika kipengele cha Muigizaji Bora wa Kiume, Dwayne Johnson alikuwa akichuana na waigizaji wengine akiwemo mtaalamu wa 007 Daniel Craig (No Time to Die), John Cena (F9: The Fast Saga), Vin Diesel (F0: The Fast Saga) na Eddie Murphy (Coming 2 America). Wengine ni Chris Pratt (The Tomorrow War), Ryan Reynolds (Free Guy), Simu Liu (Shang-Chi and the Legend of the Ten Rings). Filamu iliyompa Ushindi Johnson ni Jungle Cruise.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8ff523ee42fe6a1f2a3c3e0eb93c9d3e.png

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments