loader
Kaze: Tutawafunga

Kaze: Tutawafunga

KOCHA msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanaendeleza machungu kwa wapinzani wao Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba na Yanga ni pambano linalotarajiwa kumaliza tambo kwani kwa sasa kila upande unajitapa kuondoka na pointi tatu kutokana na ubora ambao umeoneshwa na timu zao kwenye michezo ya karibuni.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kaze alisema  yeye na bosi wake Nasriddine Nabi, wameandaa vyema kikosi chao kuhakikisha wanaendeleza furaha kwa mashabiki wa Yanga na kuzidi kujikita kileleni mwa ligi hiyo na kuwapoteza watani zao Simba.

“Maandalizi yetu yamekwenda vizuri, hatuna majeruhi, tumepania kushinda mchezo wa keshokutwa (kesho) nia na uwezo tunavyo na hii ni kutaka kutimiza malengo yetu ya kubeba mataji yote msimu huu, na hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chetu,” alisema Kaze.

Kocha huyo raia wa Burundi, alisema anatambua Simba watakuja kwa nguvu kutaka kulipa kisasi cha kuwafunga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, lakini hilo litakuwa gumu sababu kikosi chao kimekuwa kikiimarika siku baada ya siku msimu huu.

Alisema wanajua ukubwa wa mchezo huo na wao wamewaandaa wachezaji katika hali zote lengo ni kuhakikisha hawatetereki na chochote kitakachotokea uwanjani wakati mechi ikiendelea.

Kaze amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia soka safi na ushindi usiokuwa na malalamiko kutoka kwa wapinzani wao Simba, ambao wapo chini ya kocha Mhispania, Pablo Franco.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1e1971006d419c9637be9d0cacfaa5e0.jpeg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi