loader
Rais Samia amtunuku Korongo Rais Kenyatta

Rais Samia amtunuku Korongo Rais Kenyatta

 RAIS Samia Suluhu,  ametoa zawadi ya ndege aina ya Korongo 20 kwa Kiongozi wa Kenya, Rais Uhuru Kenyatta leo Ijumaa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya ahadi ya kuimarisha utalii wa pamoja kwa nchi hizo za Afrika Mashariki.

Rais Kenyatta yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi na alishiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara kama mgeni maalumu.

“Nakukabidhi vyeti vya ndege hawa naamini watafika Kenya kabla ya sherehe za X-mass baada ya kukamilisha taratibu muhimu na hiyo ndiyo zawadi yetu kwenu,” amesema Rais Samia Ikulu ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Rais Samia, Kenya ina korongo 12 dhidi ya korongo (gruidae) 4,000 walioko Tanzania. Hata hivyo wawili hao wamekubaliana kuimarisha sekta ya utalii ambayo wamekiri imeathiriwa zaidi na maradhi ya Covid 19.

                                                                                    

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fcdf6157bb5c4fc8c1d438797a2925d6.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi