TIMU ya netiboli ya Songwe imeanza kwa kishindo katika mashindano ya kombe la Taifa yaliyoanza jana baada ya kuichapa Simiyu kwa magoli 68 16, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo mwingine Tanga iliifunga Kaskazini Unguja kwa magoli 44-37 na Morogoro ikaifunga Ruvuma kwa 28-25.
Nayo Tabora iliifunga Kusini Unguja kwa magoli 45 -6, Pwani ikaifunga Geita kwa magoli 49 -41.
Katika matokeo ya mchezo wa soka kwa wanawake uliochezwa Uwanja wa Karume, Ilala, Unguja Magharibi wamechairaza Katavi mabao 3-0 na Rukwa wameichakaza Kaskazini Unguja kwa mabao 4-1 kwenye uwanja wa Gwambina.
Katika uwanja wa Uhuru mchezo wa kwanza kati ya Dar es Salaam na Iringa haukuchezwa kwa sababu ambazo hazikujulikana.
Aidha, michezo ya Pwani dhidi ya Mwanza na Kusini Unguja na Dodoma haikuchezwa kwa vile Mwanza na Dodoma hazijafika Dar es Salaam
Mashindano hayo ambayo yanashirikisha michezo ya riadha, netiboli na soka kwa wanawake na wanaume yanatarajiwa kuhitimisha Desemba 16.