loader
Masanja amvunja mbavu Rais Samia

Masanja amvunja mbavu Rais Samia

MCHEKESHAJI Emanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ juzi alimuacha hoi na kumvunja mbavu Rais Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru kwa vituko vyake.

Pamoja na kauli nyingi za mizaha alizozungumza kwenye uwanja wa Uhuru siku hiyo, Masanja alimvunja mbavu zaidi rais Samia na wageni wengine uwanjani hapo alipomwambia (Rais) kama atajenga uwanja wa mpira wa kisasa mkoani Dodoma hata wajane wataenda Kombe la Dunia.

Masanja ambaye alikuwa anatumia sanaa ya uchekeshaji kufikisha ujumbe alisema, kama Uwanja wa Uhuru na Benjamin Mkapa, timu ya Taifa ya soka la watu wenye ulemavu, Tembo Warriors wamefuzu

Kombe la Dunia hata uwanja mkubwa ukijengwa Dodoma wajane wote wataenda katika michuano hiyo ya dunia.

“Fikiria tuna uwanja huu walemavu wameenda Kombe la Dunia, sasa tukikamilisha na ule wa Dodoma wajane wote wataenda pia,”alisema maneno hayo yaliyomfurahisha Rais Samia na kucheka.

Kama ilivyo kawaida ya mchekeshaji huyo aliingia uwanjani kutamba na sanaa yake akiwa amevaa wigi la ‘afro’ na viatu vya zamani aina ya Raizoni kuonesha dhahiri kuwa ule ulikuwa muonekano wa kuchekesha.

Mbali na hayo, msanii huyo alimsifia Rais Samia akisema ndani ya miaka 60 ya Uhuru wamekuwa wakiishi kwa burudani hakuna kusikia vimbunga wala nzige wakisumbua zaidi ya kusikia nchi nyingine.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c7d20f5c3341fc061688372b4aca75cb.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi