loader
Mtibwa yazindukia Manungu

Mtibwa yazindukia Manungu

TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Biashara United kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.

Mtibwa Sugar ambayo imefikisha pointi tano baada ya ushindi huo katika raundi ya nane kwenye michezo iliyopita ilikuwa na sare mbili na kufungwa michezo mitano na kupanda hadi nafasi ya 15 kutoka mkiani.

Katika mchezo huo Mtibwa Sugar ilipata bao la kwanza dakika ya 13 kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Nzigamasabo Styve baada ya mshambuliaji Salum Kihimbwa kuangushwa katika eneo la hatari na kudumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na Mtibwa Sugar kuongeza bao la pili lililofungwa na Said Ndemla kwa shuti kali akiwa nje ya eneo la penalti akiunganisha pasi ya Baraka Majogoro na kumshinda kipa wa Biashara United dakika ya 73.

Biashara United ilionekana kuidharau Mtibwa Sugar kwani haikufanya shambulizi lolote la maana na kujikuta wakifunga. Kwa matokeo hayo Biashara inaendelea kubaki na pointi zake nane katika nafasi ya 11 baada ya kucheza michezo minane, ikishinda mchezo mmoja, sare tano na kufungwa michezo miwili.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 20 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 18, Mbeya City ya tatu ikiwa na pointi 14 sawa na Polisi Tanzania inayoshika nafasi ya nne zote zikiwa zimecheza michezo minane.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/9f59a1c496f82cd9eeadc2ea16d85fb5.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Na Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi