loader
Tanzania kidedea mashindano ya ubunifu Finland

Tanzania kidedea mashindano ya ubunifu Finland

MBUNIFU kutoka nchini Tanzania Godfrey Kilimomweshi, ameibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Kimataifa ya kunadi ubunifu yanayohusisha nchi zilizopo Kusini mwa Afrika, yaliyofanyika nchini Finland mwanzoni mwa mwezi huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk Amos Nungu alisema hayo alipozungumza na waandishi wa Habari kuhusu ushindi huo wa Tanzania.

Dk Nungu alisema kwa miaka minne sasa Tanzania imekuwa ikishiriki katika Program ya Kukuza Ubunifu Kusini mwa Afrika inayofadhiliwa na serikali ya Finland kwa kushirikiana na nchi tano.

Alitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Botswana, Namibia, Afrika Kusini na Zambia.

" Kila mwaka program hii huandaa mafunzo ya kukuza ubunifu kwa wabunifu Watano wa nchi zinazoshiriki.

"Mafunzo hayo huambatana na mashindano ambapo mshindi hupata fursa mbalimbali za kuendelezwa katika nyanja ya ubunifu,"alisema.

Alisema kati ya wabunifu 11 walionadi ubunifu wao, Kilimomweshi aliibuka mshindi wa kwanza.

Alisema Kilimomweshi amebuni mfumo wa simu unaowawezesha wenye nahitaji ya fundi kupata huduma ya upatikanaji wa mafundi kupitia simu ya kiganjani.

Naye Kilimomweshi ameshukuru Tume hiyo kwa kazi wanayoifanya ya kuwatafuta wabunifu, kuwasaidia na kuwajenga.

Alihamasisha vijana kujitokeza kwenye fursa mbalimbali zinazotokea. 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ebcf404276085771b1b5299726a9fdb7.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Na Lucy Ngowi              

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi