loader
DAR, MARA NUSU FAINALI KOMBE LA TAIFA

DAR, MARA NUSU FAINALI KOMBE LA TAIFA

TIMU za mchezo wa soka za wanaume za Mara na Mjini Magharibi zimefuzu nusu fainali wakati soka la wanawake timu ya mkoa wa Dar es Salaam nayo imekuwa ya kwanza kufuzu kuingia nusu fainali katika mashindano ya Kombe la Taifa yanayofanyika Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Yusuph Singo alisema michezo ya riadha na sanaa itaanza kurindima leo. “Kwa mara ya kwanza mikoa inayoshiriki mashindano haya imethibitisha kushiriki michezo mingi iliyopo ndani ya riadha,” alisema Singo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Mashindano hayo, Jackson Ndaweka alisema mikoa 24 imethibitisha kushiriki, kati ya hiyo 19 ni kutoka Tanzania Bara na mitano Zanzibar. Alisema jumla ya michezo 18 itashindaniwa katika mashindano hayo, huku hatua ya nusu fainali ya mashindano ya netiboli na soka inapigwa katika viwanja tofauti. Kwa upande wa soka la wanawake, Dar es Salaam imekuwa ya kwanza kukata tiketi ya nusu fainali baada ya kuichapa Mjini Magharibi kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa jana.

Timu ya wanaume ya Mara na Mjini Magharibi zimefanikiwa kutinga nusu fainali, Mara imepata nafasi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manyara, wakati Mjini Magharibi imeichapa Kusini Unguja mabao 3-0. Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sanaa, Leah Kihimbi alisema katika sanaa itakuwepo miziki ya kizazi kipya pamoja na Singeli.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/72aa4e9eda059710a5555be7bbe7be2f.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Na Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi