loader
Kaze aonya wachezaji Yanga

Kaze aonya wachezaji Yanga

KOCHA Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amewataka wachezaji wa timu hiyo kuziheshimu timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu, vinginevyo wanaweza kujikuta wanatoka patupu msimu huu.

Yanga inaongoza ligi kwa sasa lakini timu hiyo inashikilia rekodi mbaya kwa kumaliza misimu minne bila kubeba taji hilo na kuwaachia watani zao Simba wakilimiliki wanavyotaka.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kaze alisema amegundua baadhi ya wachezaji wao wamekuwa wakidharau baadhi ya mechi wanapocheza na timu ndogo kitu ambacho ni kibaya na kinaweza kuwagarimu na kujikuta wanashindwa kufikia malengo yao.

“Yanga inamalengo yake na malengo hayo yanafikiwa kutokana na juhudi za wachezaji uwanjani sasa nilazima tuwakumbushe hizi kila mchezo lazima wacheze kwa kujitoa siyo kuchagua mechi ya kucheza kwabidii na nyingine unacheza ilimradi,” alisema Kaze.

Kocha huyo alisema bidii za uongozi na benchi a ufundi limepania kufuta unyonge msimu huu kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA hivyo vinaweza kutimia endapo kila mtu atawajibika ipasavyo kwenye nafasi yake.

Alisema asilimia kubwa ya wachezaji wao wanacheza kwa kujitoa lakini wapo baadhi yao nikama wanachagua mechi tayari wamewaita kuzungumza nao na anaamini watabadilika na kufuata maelekezo yao ili kutimiza kile walichokikusudia mwishoni mwa msimu huu.

Yanga imedhamiria kufanya mambo makubwa msimu huu ikiwemo kutwaa mataji yote ya ndani ambayo yanashikiliwa na watani zao Simba na hiyo imetokana na usajili walioufanya kwa kusajili nyota wenye uwezo na majina makubwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2ab3803c10abe617835b58b2e1fc5cae.jpeg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi