loader
Kashfa ya ngono yamuibua Eto’oo

Kashfa ya ngono yamuibua Eto’oo

SAMUEL Eto’o amewasimamisha kazi Ofisa wa Benchi la Ufundi la timu ya Taifa ya Cameroon ‘Indomitable Lions’, Ferdinand Makota kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na kashfa ya ngono.

Katika barua, Eto’o, ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Kandanda Cameroon, Fecafoot, alimkumbusha Makota jukumu la kuwa na tabia ya mfano.

Makota alikuwa ofisa wa timu ya soka ya wanaume ya Cameroon, Indomitable Lions.

“Kwa hiyo, nawajulisha kuanzia leo na mpaka itakapotangazwa tena, utasimamishwa kazi yako ya mratibu msaidizi wa timu ya Taifa ya Cameroon ‘Indomitable Lions’,” Samuel Eto’o aliandika.

Barua ya Eto’o inakuja siku chache baada ya picha za mapenzi za Makota kuonekana kwenye mitandao ya kijamii.

Hatua hiyo imekuja wiki moja kabla ya kuanza kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, ‘Afcon 2021’ ambalo nchi hiyo ya Afrika ya Kati ni mwenyeji wa mashindano hayo yatakayoanza Januari 9 na kumalizika Februari 6.

foto
Mwandishi: YAOUNDÉ, Cameroon

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi