loader
Tanzania yapokea uwekezaji Dola bilioni 1/- mwaka 2020

Tanzania yapokea uwekezaji Dola bilioni 1/- mwaka 2020

Tanzania imepokea uwekezaji wa Dola bilioni 1 kutoka nje ya nchi kwa mwaka 2020 licha ya uwepo wa janga la UVIKO-19.

Takwimu hizo zimetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 4, 2022 wakati akizungumza Ikulu Dar es Salaam katika mapokezi ya taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Aidha, Majaliwa amesema kuwa mwezi Disemba, 2021 Serikali ilivunja rekodi ya makusanyo ya kodi kwa kukusanya Sh trilioni 2.51 sawa na 109% wa lengo la kukusanya trilioni 2.29 katika kipindi hicho kwa mwaka  uliopita. 

Katika upande mwingine, Waziri Majaliwa amesema mpaka kufikia juni 2022 miradi yote ikiwemo ya Afya, Maji, Elimu, Maliasili itakuwa imekamilika kama ilivyopangwa.

“Utekelezaji wa miradi hii umeleta manufaa makubwa kwa Jamii yetu, si tu kwa kupata miundombinu ya kutolea huduma bali pia Jamii imefaidika ikiwemo katika kuongeza ajira, pato la wananchi na kipunguza umasikini,” amesema Waziri Majaliwa.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f32a7d6ed60b9c60a3fc09dc150e381b.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi