loader
Kaze atamba kutetea kombe

Kaze atamba kutetea kombe

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema kuwa ushindi walioupata wa mabao 2-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe Uwanja wa Amani ni mwanzo mzuri katika kutetea kombe hilo.

Yanga mabao yake yalifungwa na Heritier Makambo dakika ya 32 kwa shuti kali akitumia vyema pasi ya Zawadi Mauya bao la pili likifungwa na Denis Nkane dakika ya 49 alipomalizia krosi ya Dickson Ambundo.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kuongoza kundi B ikiwa na pointi tatu sawa na KMKM wakipishana kwa idadi ya mabao ya kufunga huku Taifa Jang’ombe, wakiondoshwa mashindanoni baada ya kufungwa michezo yote miwili.

Akizungumza juzi baada ya mchezo huo Kaze alisema Jang’ombe ni timu nzuri wanajituma kipindi cha kwanza kwa kujaribu kuziba njia lakini ubora wao uliwapa matokeo.

“Ni jambo zuri kuanza na ushindi katika mchezo wa kwanza inakupa nguvu kwenye mchezo wa pili dhidi ya KMKM ambao naamini hautakuwa rahisi,” alisema Kaze.

Kocha wa Taifa Jang’ombe, Omary Hamis, alisema ubora wa Yanga hasa eneo la katikati na wao kushindwa kutumia nafasi kuliwapa nafasi kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

“Ulikuwa mchezo wetu wa mwisho katika mashindano ya Mapinduzi tumeondoshwa, sasa tunajipanga na michezo ya Ligi Kuu ya Zanzibar,” alisema.

Katika mchezo huo kipa wa Taifa Jang’ombe, Hussein Abel aliibuka mchezaji bora akakabidhiwa Sh 500,000.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7109230e42470f2845476081533074e9.jpeg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi