loader
Ni vita Afcon Cameroon

Ni vita Afcon Cameroon

MASHINDANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanaanza leo nchini Cameroon kwa wenyeji kucheza na Burkina Faso kwenye Uwanja wa Yaounde Olembe saa 10:00 jioni na mchezo mwingine utakuwa dhidi ya Ethiopia na Cape Verde saa 1:00 usiku.

Mashindano haya ya 33 yanaanza leo hadi Februari 6 yakishirikisha mataifa 24 ambayo yatashindana katika makundi sita katika miji mitano nchini humo.

Kesho Kundi B, Senegal itacheza na Zimbabwe Stade de Kouekong, Bafoussam saa 7:00 mchana na Morroco itaivaa Ghana katika Uwanja wa Stade Ahmadou Ahidjo,Yaoundé kuanzia saa 10:00 jioni.

Nyota wa Ligi Kuu ya England na Ulaya watakuwa dimbani kutetea mataifa yao kama Mohamed Salah, Sadio Mane, Riyad Mahrez Awali mashindano hayo yalikuwa yachezwe Juni 2021 lakini yalibadilishwa hadi Januari kuepuka msimu wa mvua nchini Cameroon lakini pia yaliahirishwa hadi 2022 kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Mpira unaotumiwa ni Umbro Toghu, uliopambwa na rangi za mavazi ya asili maarufu nchini Cameroon. Mechi zote 52 zitakuwa na waamuzi wasaidizi wa video (VAR) kwa mara ya kwanza wakati katika mashindano ya 2019 nchini Misri teknolojia hiyo ilianza kutumika kwenye robo fainali.

Caf imechagua waamuzi wa kati 24, wasaidizi 31 na waamuzi wasaidizi wa video nane kutoka nchi 36 kwa ajili ya mashindano hayo. Bingwa atapata fedha zawadi ya Dola za Marekani milioni 5, ongezeko la dola 500,000 kutoka 2019 ambazo ni sawa na Sh Bilioni 11, 500,000,000.

Mshindi wa pili atapata dola milioni 2.75, sawa na Sh Bilioni 6.325 wakati timu zilizofungwa nusu fainali waliopigwa na robo fainali watapokea dola milioni 2.2 sawa na Sh Bilioni 5 na dola 1.175 sawa na Sh Bilioni 2 kwa mtiririko zawadi ambazo zimeongezeka kwa dola milioni 1.85 kutoka 2019.

foto
Mwandishi: YOUNDE, Cameroon

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi