loader
Mane aibeba Senegal Afcon

Mane aibeba Senegal Afcon

PENALTI ya dakika za majeruhi iliyopigwa na mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Sadio Mane imeipa ushindi wa kwanza timu yake ya taifa ya Senegal iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Kouekong, Cameroon.

Senegal walipata penalti hiyo baada ya mchezaji Kelvin Madzongwe kuushika mpira ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru pigo hilo na Mane kuukwamisha mpira wavuni.

Kocha Aliou Cisse wa Senegal, inayoshika nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa mchezo wa soka barani Afrika na 20 duniani, iliingia katika mchezo huo bila wachezaji wawili kipa namba moja, Edouard Mendy na beki Kalidou Koulibaly ambao walikutwa na virusi vya Covid-19.

Kukosekana kwa nyota hao hakukuwa na madhara kwa Simba hao wa Milima ya Teranga, kwani walitengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini wakashindwa kufunga.

Senegal walipaswa kupata bao dakika ya kwanza ya mchezo baada ya shuti la umbali mrefu la Bouna Sarr kwenda nje kidodo ya lango.

Mshambuliaji Sadio Mane, alipata nafasi nzuri alipojaribu kukontroo mpira akiwa umbali wa yadi 30 na kisha kupiga shuti lililookolewa na kipa Petros Mhari.

Kipindi cha pili, Abdou Diallo,karibu aipatie timu yake ya Senegal bao, lakini kichwa cha kuokoa kilichopigwa na beki wa kati kilitoa hatari katika lango la kipa Mhari.

Baada ya mchezo huo staa huyo wa Senegal, alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kwa kuibeba timu yake kupata ushindi wa kwanza katika Kundi B.

Mashindano hayo yanaendelea tena leo kwa mechi za Kundiwakati Nigeria watakwaana na Misri katika mchezo utakaofanyika kuanzia saa 10 jioni na Sudan dhidi ya Fuinea Bissau usiku.

foto
Mwandishi: BAFOUSSAM, Cameroon

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi