loader
Mbeya City yaipumulia Simba SC

Mbeya City yaipumulia Simba SC

ZIMEBAKI pointi mbili, Mbeya City iwafikie Simba SC katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, baada ya timu hiyo kushinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sokoine Mbeya leo.

Aziz Andambwile alifunga bao hilo dakika ya 55, akiunganisha mpira wa kona na kuifanya timu hiyo kukusanya pointi sita katika michezo miwili ya mwisho ukiwemo ushindi bao 1-0 dhidi ya Simba SC.

Ushindi huo unaendelea kuiweka Mbeya City katika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya Simba SC kwa pointi mbili. Timu hiyo ina pointi 22 wakati Simba imekusanya 24 huku ikiwa na michezo miwili mkononi.

Haikuwa siku nzuri kwa Ruvu Shooting baada ya Abdulsamad Kassim kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 56 kufuatiwa kumfanyia madhambi Aziz Andambwile.

Dakika ya 65, Ruvu Shooting walikosa penalti na kuua matumaini ya walau kupata sare katika mchezo huo.

Hali ya Ruvu imezidi kuwa mbaya baada ya kupoteza michezo minne na sare mbili katika michezo sita ya mwisho waliyocheza na kufanya kushika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 11 katika msimamo wa ligi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fc6d0990d94a1b2cd8d0c7d489401ea7.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi