loader
Hapi atoa saa 48 kwa Nassari

Hapi atoa saa 48 kwa Nassari

HALMASHAURI ya Bunda mkoani Mara imetumia Sh milioni 60 kujenga msingi wa jengo moja kati ya majengo sita ya kituo cha Afya Isanju tangu Septemba mwaka jana.

Bunda ilipokea Sh milioni 250 kukamilisha ujenzi wa majengo hayo ndani ya kipindi cha miezi minne, hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ali Hapi amebaini kuwa ujenzi huo bado uko katika hatua ya msingi.

Kufuatia ukaguzi huo, Hapi ametoa saa 48 kwa uongozi wa Halmashauri hiyo inayoongozwa na Joshua Nasari kupeleka majina ya wakuu wa idara wanao kwamisha mradi huo.

 “Fedha zikiingia tu, wanafungulia mirija ya matumbo yao mpaka yashibe ndiyo miradi itekelezwe, haikubaliki," amesema Hapi na kusisitiza majina hayo yatapelekwa Tamisemi ili wapangiwe kazi zingine.

Fundi Mkuu wa Ujenzi huo, Robert Mwijarubi amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa chanzo ni kutopelekwa kwa vifaa kwa wakati.

Amesema halmashauri hiyo imemsumbua kuliko zote  hata katika ujenzi wa  madarasa  chanzo kikiwa ubinafsi wa baadhi ya wakuu wa Idara zikiwemo za Fedha, Manunuzi na Mipango.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya hiyo, Joshua Nassari amesema alikuta baadhi ya watumishi wakilipa fedha kwa ajili ya vifaa na havyo na havichukuliwi hata kwa mwaka mzima, kwa kisingizio cha kutokuwa na stoo.

"Kuna Sh milioni 400 zililipwa mahala tangu Machi Mwaka jana na vifaa vilivyolipiwa havijachukuliwa mpaka sasa, tunazifatilia ili kuzirejesha halmashauri," amesema Nassari.

 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/80a9cafacb6368f1d760de84b9dabeb8.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Editha Majura, Bunda.

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi