MIFUGO 1,257 imepoteza maisha kutokana na kukosa maji na malisho katika mkoa wa Kilimanjaro
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai wakati akitoa taarifa ya Mkoa huo kwa Rais Samia Suluhu, katika uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni.
Kagaigai ametaja mifugo hiyo iliyokufa kuwa ni ng’ombe 841, kondoo 406 na punda 10
"Mweshimiwa Rais, pamoja na mafanikio na kazi mbalimbali za maendeleo zinazoendelea, Mkoa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutonyesha kwa mvua za vuli, hali ambayo imesababisha ukame na vifo vya mifugo.
" Uongozi wa mkoa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na hali hiyo. Pamoja na vifo hivyo vya mifugo, hali ya chakula bado ni nzuri, na Mkoa unachakula cha kutosha” amesema Kagaigai.